NA HADIJA OMARY, MATUKIODAIMAAPP LINDI
ILI kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma bora za Afya Bank ya NMB kwa kushirikiana na Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa (NHIF) kupitia mpango wake wa Ushirika Afya Imeanza kutoa Mkopo wa Bima za Afya kwa wakulima Mkoani Lindi.
Hayo yamesemwa na Meneja wa Bank hiyo Kanda ya kusini Janeth na Shango wakati wa ghafla fupi ya kukabidhi meza 50 na viti 50 vyenye thamani ya shilingi milioni tano kwa shule ya secondary Mkopwe kata ya Nachunyu halmashauri ya Mtama Mkoani Lindi.
Shango alisema uamuzi wa kutoa mikopo ya Bima ya Afya kwa wakulima hao ni baada ya kuona kwamba kundi hilo limekuwa halina kadi hizo hali iliyopelekea kupata changamoto ya kupata huduma za Afya.
Alisema ili kuhakikisha adhima ya Nchi kuona kila Mwananchi wake anapata huduma bora za Matibabu wao kama wadau muhimu wameona ipo haja ya kulisaidia kundi la wakulima ambalo kwa kiasi Fulani wamekuwa wakishindwa kupata hela ya moja kwa moja kwa ajili ya kujiunga na mfuko huo.
“sasa kwa sababu wakulima wengi wapo kwenye ushirika tukaamua kuingina ubia na vyama vyenu vya ushirika hivyo mwananchi yeyote ambae ni mwanachama wa chama cha ushirika bila kujali unatoka Bank gani unaweza kupatiwa huma hiyo bila riba yoyote” Alieleza Shango.
Hata hivyo Shango alisisitza kuwa pamoja na kutambua jitihada zinazofanywa na Serikali ya awamu ya sita katika kutatua changamoto mbali mbali katika Sekta ya Elimu na Afya wao kama wadau pia wanao wajibu wa kuunga mkono jitihada hizo Ambapo Bank hiyo kwa mwaka 2022/2023 imetenga kiasi cha shilingi bilioni mbili kwa ajili ya kusaidia katika sekta hizo.
Aidha kuhusu vifaa walivyovitoa Shango alieleza kuwa meza na viti hivyo waliyoyakabidhi ni moja ya ushiriki wao katika maendeleo ya jamii na wao kama Bank wanao wajibu wa kuhakikisha jamii inayowazunguka inanufaika kutokana na faida wanayoipata.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndanga akizungumza wakati wa kupokea Msaada huo , alitumia fursa hiyo aliwataka wakulima Wilayani humo kuchangamkia fulsa ya Mikopo ya Bima ya Afya ya Taifa (NHIF) inayotolewa na Bank ya NMB ili kuwa na uhakika wa matibabu pindi wanapougua .
Ndemanga alisema licha ya kuwa na uhakika wa kupata matibabu pindi wanapougua pia ni moja ya ishara ya kutambua mchango unaotolewa na Bank hiyo katika jamii yao.
Alisema kuwa ni wazi kwamba ugonjwa hauna hodi kwa kuangalia kwa kuangalia kipindi ambacho unapesa au laah lakini unaweza kuwa na uhakika wa kupata matibabu wakati na mahali popote Endapo utakuwa na Bima ya Afya.
“Changamoto kubwa mliyokuwa nayo watu wa huku pamoja na uzalishaji mkubwa na hela nyingi mnazopata kutokana na kilimo lakini swala la kukata bima sio kipaumbele chenu matokeo yake mnapoishiwa na hela unaanza kuumwa ukiwa huna hela”.
“yupo mzee mmoja hapa nachunyu simtaji kwa jina ila mwenyewe anajijua msimu uliopita alipata milioni 42 mwezi oktoba lakini ulipofika mwezi januari Mwishoni hana hata shilingi moja na anaumwa anaanza kuhangaika kuata matibabu , sasa natoa mifano ya kweli ili mjue umuhimu wa bima" alisema Ndemanga.
Kwa upande wake mmoja wa wazazi walioudhuria kwenye ghafla hiyo Bi. Zuhura Saidi alisema utaratibu huo utakuwa mkombozi kwa wakulima kwani Mkulima sasa hatakuwa na mawazo tena ya kufikiri atapata wapi pesa ya kugharamia matibabu pindi atakapougua.









0 Comments