Header Ads Widget

YOUNG SCIENTISTS TANZANIA (YST) YAWAPIGA MSASA WALIMU WA MASOMO YA SAYANSI LINDI

 


NA HADIJA OMARY,MATUKIO DAIMAAPP,

LINDI

Mwanzilishi mwenza wa taasisi ya wanasayansi chipukizi  YOUNG SCIENTISTS TANZANIA (YST)  Dr. Gozibert Kamugisha amesema uwekezaji katika masomo ya Sayansi  ni miongoni mwa njia ya kulifikisha Taifa lolote hapa ulimwenguni katika maendeleo endelevu.


Dr. Kamugisha ameyasema hayo wakati wa mafunzo kwa walimu wa Shule za Sekondari Mkoa wa Lindi yaliyolenga kuwapa ujuzi wa namna gani ya kuweza kuwafundisha wanafu jinsi ya kufanya utafiti kulingana na matatizo ama changamoto zilizopo katika jamii zao kwa kutumia ujuzi wa Sayansi wanayofundishwa Darasani kwa Masomo ya Fizikia Baiolojia na Kemia.



Mafunzo hayo yaliyofanywa na taasisi hiyo ya yamefadhiliwa na kampuni ya shell Tanzania yamefanyika katika shule ya sekondari lindi kwa  kuwakutanisha walimu 41 kutoka Halmashauri za Kilwa, Mtama, Manispaa ya Lindi, Ruangwa na Liwale Mkoani Lindi.


alisema kuwa ni wazi kuwa nchi zote zilizopata maendeleo Duniani  ziliwekeza katika masomo ya sayansi na Teknolojia hivyo Tanzania kama Nchi inayoendelea haina budi kuwekeza katika masomo hayo kwa vijana ili kuijuaZaidi Sayansi na atimae kuweza kufanya gunduzi na teknolojia ambazo zitaweza kusukuma maendeleo ya Nchi


“Sisi kama taasisi tumeamua kujikita kwa vijana wanaosoma masomo ya Sayansi kwa sababu ukiangalia nchi zote zilizoendelea zinafanya uwekezaji mkubwa kwa vijana walioko shule za Sekondari kwa kushirikiana na viwanda mbali mbali kuweza kuwafundisha wanafunzi kuweza kujifundisha katika ugunduzi hivyo kama Tanzania  tunataka kuwa na Taifa endelevu hakuna njia ya mkato lazima tuwekeze vya kutosha  katika sayansi”.


Kwa upande wake mwakilishi wa katibu Tawala Mkoa wa Lindi, katibu tawala Msaidizi mipango na uratibu juhudi mgala alisema kuwa mafunzo hayo yatakuwa msaada mkubwa kwa wanafunzi na vijana wanaosoma masomo ya sayansi katika Mkoa huo wa Lindi.


“ukiangalia mfumo unawataka wanafunzi waweze kufanya utafiti katika mazingira yao wanayoishi kwa hivyo kadili muda unavyozidi kwenda wanafunzi hawa kwa miaka minne mitano tunategemea wataingia vyuo vikuu hivyo ni matarajio yetu kuwa kwenye tafiti ambazo watakuwa  wameanza kuzijenga tangu wakiwa msingi watakapofika vyuo vikuu watakuwa wazuri kwenye utafiti."


“Pamoja na hayo mwanafunzi anaweza kugundua vitu mbali mbali mfano mwanafunzi anachangamoto Fulani pale nyumbali kwao labda shamba la Baba ake linawadudu wanaingia kwa kutumia ujuzi atakaofundishwa na walimu hawa anaweza kufanya utafiti na hatimae kuweza kutibu tatizo hilo ”.


Nae Beatrice Mbawala  Mwalimu wa Shule ya Sekondari kibutuka Wilayani Liwale alisema kuwa pamoja na kwamba Walimu hao wamekuwa wakifundisha masomo ya Sayasi kwa wanafunzi lakini zipo changamoto za kimifumo ambazo zinachangia moja kwa moja kukwamisha ama kuwafanya wanafunzi kushindwa kufanya utafiti licha ya kusoma masomo hayo ya Sayansi


Alisema changamoto hizo ni pamoja na njia za ufundishaji ambapo mara nyingi wanafunzi wamekuwa wakisoma kwa nadhalia pasipo kufanya kwa vitendo kwa yale masomo aliyosoma darasani kuona kwa vitendo na namna yanavyotumika au kufanyika katika mazingira ya kawaida




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI