Header Ads Widget

MOI KUHUDUMIA WANANCHI KATIKA MAONYESHO YA SABASABA 2022

 



Dar es Salam


TAASISI ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI), imeanza rasmi kutoa huduma ya bure kwa watu mbalimbali wanaotembelea  katika Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara maarufu Sabasaba ambayo msimu huu ni ya 46.


Akizungumzia huduma hizo ambazo zimeanza rasmi mapema leo Julai Mosi, Msemaji wa MOI, Patrick Mvungi alisema 


"Katika maonesho ya sabasaba mwaka huu tunatoa huduma za kibingwa za ushauri kwa magonjwa ya mifupa, ubongo, mgongo, mishipa ya fahamu,Tiba lishe, mazoezi tiba pamoja na viungo saidizi”.


Mvungi ametoa wito kwa washiriki wa maonesho ya sabasaba kutembelea banda la MOI katika hema la Jakaya Kikwete ili wapate huduma bila gharama yoyote


"Watu wote wanakaribishwa kutembelea banda la MOI ndani ya hema kubwa la Jakaya Kikwete ndani ya Sabasaba



..Watapata huduma hizo tajwa za kibingwa na pia watapata maelezo mbalimbali kuhusu huduma zitolewazo na MOI." Alisema Mvungi.


Aidha, huduma hizo zitaendelea hadi mwisho wa maonyesho hayo lengo likiwa kusaidia jamii


MOI ni Taasisi pekee hapa nchini ambayo imebobea katika matibabu na upasuaji wa ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI