Na Gabriel Kilamlya MATUKIO DAIMAAPP,NJOMBE
Mkulima mkubwa wa parachichi katika mtaa wa Maheve kata ya Ramadhani mjini Njombe Steven Nemes amemhoji Mbunge wa jimbo la Njombe mjini juu ya maneno yanayoelezwa mitaani juu ya uwepo wa mikopo ya kilimo kwenye taasisi za fedha ilihali hakuna fedha zinazotolewa.
Nemes amemhoji mbunge huyo alipozulu katika mtaa wa Maheve kwa ziara ya kijimbo ambapo amemtaka mbunge huyo kumweleza kama mmoja wa watunga Sera na sheria juu ya taarifa za uwepo wa mikopo hiyo kwa wakulima ilihali kila akifuatilia kwenye taasisi hizo anaambiwa hakuna mikopo hiyo.
Amesema hata kwenye Benki ya kilimo pia ameelezwa hakuna mikopo hiyo jambo ambalo linampa wakati mgumu katika kuendeleza kilimo cha parachichi wakati wabunge na hata madiwani wamekuwa wakiwaeleza kuwa mikopo hiyo ipo.
Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Njombe mjini Deo Mwanyika ameahidi kwenda kulifuatilia suala hilo kwani hata benki ya kilimo inapaswa kutoa mikopo mikubwa na ya kati kwa wakulima wenye uhitaji.
Mbunge Mwanyika amesema wakati akitarajia kwenda kulifanyia kazi suala hilo wananchi waendelee kujiunga kwenye vikundi na kuomba mikopo isiyo na riba inayotolewa na Halmashauri kote nchini.









0 Comments