Teddy Kilanga MATUKIODAIMA APP ARUSHA
Maombi madogo ya jinai 1/2022 yaliyotolewa na Peter Michael Madeleka dhidi ya jamhuri ya kumuondoa hatiani kutokana na hukumu ya kesi ya ujuhumu uchumi namba 40/2020 imehairishwa hadi Julai 13,2022.
Kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 40/2020 iliyoamuliwa kwa njia ya makubaliano Kati ya mshtakiwa na Mwendesha Mashtaka wa Serikali nje ya mahakama na kupelekea Wakili Peter Madeleka kutoa kiasi cha Tsh Mil 2 juu ya Makubaliano hayo na faini ya laki mbili kutoka kwa Mahakama.
Akitoa maamuzi madogo kutokana na wakili mwandamizi wa serikali kutofika kwa wakati pamoja na kutoa maombi ya kuhairishwa kwa kesi hiyo katika mahakama ya hakimu mkazi, Hakimu Herieth Mhenga alisema kuwa kimsingi kesi hiyo imepangwa kwa muda mrefu na inaumuhimu kama kesi nyingine hivyo inahaki ya kusilizwa.
Aidha alisema ni vyema pande zote zimepewa haki ya kusikilizwa ijapokuwa sababu za kuhairishwa kwa kesi hazitoshelezi hivyo ameruhusu maombi hayo lakini kwa mara ya mwisho na isijirudie tena kwa wakati mwingine.
"Nimepokea maombi lakini suala hili lililojitokeza lisijirudie kwani kucheleweshwa kwa kesi ni ucheleweshwaji wa upatikanaji wa haki hivyo naiharisha kesi hii hadi julai 13,julai 2022,"alisema Hakimu Mhenga.
Awali akiielezea mahakama sababu za kuomba kuahirishwa kwa kesi hiyo,Wakili mwandamizi wa serikali Akisa Mhando alisema siku moja kabla ya kesi alimuomba wakili Madeleka kwa njia ya simu wahiarishe kutokana na kuwepo katika kesi ya uchumi namba 4/2022 pamoja na namba 3/2022.
"Mheshimiwa samahani sina nia ya kuidanganya mahakama nilikuwepo kwenye kesi ya uhujumu uchumi namba 4/2022 pamoja namba 3/2022 ikiwa zote zilikuwa kwa muheshimiwa Fadhili Mbelwa ambaye ni hakimu mfawidhi wa mahakama hii na zilikuwa zimepangwa kwa muda sawa,"alisema
Aidha kwa saa chache mbele ya hakimu Mhenga mzozo wa hoja za kisheria zilizuka Mahakamani hapo huku wakili Peter Madeleka akilalamikia Swala hilo kwa kudai ni kinyume na sheria ibara ya 107 A kubwa ibara ndogo ya pili B ya katiba inaeleza kuwa mahakama haipaswi kuchelewesha haki bila sababu za msingi ivyo yanayotokea kwa upande wa jamhuri ni kuisababishia Mahakama kuchelewesha kutoa haki.
Akizungumza na waandishi wa habari nje ya mahakama hiyo wakili Peter Madeleka alisema kesi hiyo ya maombi madogo ipo mbele ya mahakama ya hakimu mkazi kwa ajili ya kutengua amri iliyomtia hatiani kwa kosa la uhujumu uchumi kwa njia ya makubaliano yaliyofanyika nje ya mahakama iliyofanyika Aprili 27,2021.
"Nimekuja mahakamani kwasababu utaratibu uliyotumika kufanyika pribageini ilipelekea mimi kutiwa hatiani na mahakama hii kwani haikuzingatia sheria na ulikuwa ni kinyume na mfumo wa haki jinai,"alisema Wakili Madeleka.
Aliongeza kuwa aliyepokea fedha hizo za pribageini kwenye shauri hilo kisherika kwa mujibu wa kanuni ya 21 kanuni ndogo 3(a) hakutakiwa kupokea mwendesha mashtaka(DPP) na alizipokea fedha hizo kupitia Akaunti ya DPP iliyopo BOT.
Alisema jambo lingine analolalamikia ambalo ni msingi wa maombi yake ili mahakama iweze kutengua ni kosa alilohukumiwa nalo kutokuwa kosa la uhujumu uchumi ambalo alishtakiwa nalo tangu hapo awali ambalo alipelekwa nalo mahakamani kufanya pribageini.
"Lakini nilimlipa DPP mnamo machi 30,2021 ikiwa ni takriba ni mwezi mzima kabla ya hatujafanya makubaliano haya mahakamani na wakati huo nilikuwa gerezani hali ambayo nilikosa namna yeyote,"alisema Madeleka na kuongeza kuwa.
“Sasa kilichojiri mahakamani kinasikitisha sana mimi kama mleta maombi nilikuwa nipo tayari kusikiliza shauri hili kama ilivyokuwa imepangwa lakini tumekaa mahakamani baada ya kuitwa kwenye chumba cha mahakama tangu asubuhi tukaja kuingia kwenye shauri saa saba mchana kwasababu mawakili wa serikali walikuwa hawaonekani na hata walipo onekana yalikuwa ni kinyume na amri ya mahakama ya kulitaka shauri hili leo,” Alieleza.
0 Comments