Header Ads Widget

BMH WAJITENGENEZEA KITABU CHA MWONGOZO WA DAWA

 


Na.WAF,Dodoma


Waziri wa Afya Ummy Mwalimu jana amezindua kitabu cha  Mwongozo wa wa utoaji Dawa(Benjamin Mkapa Hospital Formulary) utakaotumiwa na waandika Dawa (Prescribes), Wafamasia,Wachunguzi na Wauguzi katika hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma. 


Kitabu hicho kimekuja ikiwa ni kutekeleza wa  agizo lake la kuhakikisha dawa zinapatikana ndani ya Hospitali na kuondoa usumbufu wa wagonjwa kwenda kutafuta dawa nje ya hospitali.

 



Mwongozo huu umeandaliwa kwa kuzingatia Mwongozo wa Matibabu  Tanzania  na  Orodha  ya  Taifa  ya  Dawa  Muhimu (Standard Treatment Guideline of Tanzania and National Essential Medicine List) ambao unalenga kukuza matumizi sahihi ya dawa kwa wagonjwa wanaopatiwa matibabu  Hospitalini hapo ili kuboresha afya   zao. 


 Pia,   Mwongozo   huu   utasaidia   katika   kuongeza upatikanaji wa dawa kwenye hospitali  kwa kuwa unaainisha orodha ya dawa zinazohitajika zaidi hapo hospitalini na kuondoa wigo mpana wenye dawa nyingi ambazo huwa ni vigumu kupatikana   hapa   nchini.  


Utekelezaji   wa   mwongozo   huu utapunguza gharama zisizo za lazima kwenye ununuzi wa dawa na vifaa tiba.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI