Header Ads Widget

KATIBU WA WAZAZI MBINGA AWATAKA WANAJUMUIYA HAO KUFUATA TARATIBU ZA UCHAGUZI.

 


Na Amon Mtega, Mbinga.


KATIBU wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma Angelo Madundo amewataka Wazazi wa Jumuiya hiyo kufuata taratibu na kanuni za uchaguzi zulizowekwa ili kuepusha migongano isiyo ya lazima.


Madundo ambaye naye ni mjumbe wa  kata ya Mbambi mjini Mbinga ametoa maagizo hayo wakati akipita kuangalia mwenendo wa uchaguzi wa kuwapata Viongozi watakayo iongoza Jumuiya hiyo toka ngazi ya matawi ,Kata na Wilaya na kuendelea ngazi za juu Mkoa na Taifa.


 Katibu amesema kuwa kumekuwepo na changamoto ya baadhi ya wanajumuiya hiyo kushindwa kutambua kanuni za uchaguzi jambo ambalo limekuwa likileta migongano isiyo ya lazima ambayo hupelekea kujigawa kwenye makundi tofauti.

 

 Amesema kuwa Chama cha Mapinduzi CCM kiliziweka Jumuiya hizo na ziwe na uongozi wake kwa lengo la kutaka Chama kiwe na muunganiko wa pamoja kupitia Jumuiya zake na siyo kuwepo kwa makundi ambayo hupelekea kuwagawa wanachama.



 Amefafanua kuwa Jumuiya ya Wazazi ndiyo dura ya Chama cha Mapinduzi CCM kwa kutegemea hekima na busara ili na Jumuiya zingine ziweze kujifunza kutoka kwenye Jumuiya ya Wazazi.


Madundo amesema uchaguzi wa kuwapata Viongozi wa Jumuiya hiyo katika ngazi ya matawi na kata unaendelea vizuri katika kata 48 za Mbinga Mjini na Mbinga Vijijini.

       


      

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI