Header Ads Widget

NANENANE KUFUNGULIWA AGOSTI 2 MOROGORO

 



MAONYESHO ya Nane nane Kanda ya Mashariki yanatarajiwa kufunguliwa Agosti 2 mwaka huu mkoani Morogoro.


Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mjini Kibaha mkuu wa mkoa wa Pwani akizungumza kwa niaba ya wakuu wa mikoa inayounda Kanda hiyo amesema kuwa yatakayofanyika katika viwanja vya Julius Kambarage Nyerere.


Kunenge amesema kuwa taasisi 552 zinatarajiwa kushiriki maonyesho hayo ya Kanda ya Mashariki ambayo yataanza Julai 31 hadi Agosti 9.


Amesema kuwa maonyesho hayo ni ya 29 kwa Kanda hiyo ambapo yatazinduliwa rasmi Agosti 2 ambapo hata hivyo mgeni rasmi atatajwa baadaye.


Aidha amesema kuwa maonyesho hayo ambayo kauli mbiu yake ni Ajenda ya kumi ya thelathini Kilimo ni biashara Shiriki kuhesabiwa kwa mipango bora ya Kilimo Mifugo na Uvuvi itahusisha Wilaya 27 zenye Halmashauri 34.


Kanda hiyo inaundwa na mikoa minne ambayo ni Dar es Salaam, Pwani, Tanga na wenyeji Morogoro.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI