Header Ads Widget

JAMII YASHAURIWA KUJIJENGEA MAZOEA YA KUSOMA VITABU NA MACHAPISHO.

 


Na Gabriel Kilamlya NJOMBE


Ili kujikomboa kifikra kwa wa Afrika wengi duniani wito umetolewa kujijengea mazoezi ya kusoma vitabu na machapisho mbalimbali kwani hii inasadia sana kukuza uelewa na maarifa ya kukabiliana na changamoto za maisha.


Katika uzinduzi wa kitabu cha FATINAH kilichoandikwa na mwandishi Gwamaka Mwamasage ambaye ni Afisa wa jeshi la polisi mkoa wa Njombe chenye maudhui ya mikasa mbalimbali ya maisha Amesema lengo la kuandika kitabu hicho ni kutaka kuiamsha jamii katika kujijengea mazoea ya kusoma vitabu ambavyo vimekuwa na elimu kubwa ndani yake ambayo haifikiwi.



Akizindua kitabu hicho mjini Njombe Mwandishi wa riwaya   takribani  40 Bwana Richard Mwambe ambaye ni mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la ''Kitabu Maisha''anakiri kuwa Watanzania wengi wamekuwa hawana mazoea ya kusoma vitabu kutokana na mapinduzi ya Teknolojia.


Kitabu cha Fatinah kimeingizwa sokoni hivi sasa ambapo baadhi ya wananchi waliofanikiwa kununua nakala hiyo wakiwemo maofisa wenzie wa Jeshi la polisi wamekiri kuwa kitabu hicho kitasaidia sana kukuza lugha ya kiswahili pamoja na kuielimisha jamii.



Riyawa ya Fatinah ya Bwana Gwamaka Mwamasage imeendelea kuchagiza kwa kiasi kikubwa katika usambaaji wa Lugha ya kiswahili Duniani.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI