Header Ads Widget

HAIKUWA BAHATI MBAYA KUJIUNGA SUK-ATC :OTHMAN

NA,MATUKIODAIMAAPP,SMZ

MAKAMO Mwenyekiti wa Chama cha ACT wazalendo Othman Massoud Othman amesema  uamuzi wa chama hicho kuingia kwenye Serikali ya Umoja wa kitaifa Zanzibar (SUK) ulikuwa na lengo la kuikwamua nchi hiyo kutoka kwenye hali mbaya ya kisiasa na kiuchumi.

Othman aliyasema hayo huko Tungu Mkoa wa Kusini Unguja wakati akifungua Afisi mpya ya chama hicho huko Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja leo Julai 23,2022.

Alisema mambo yanaendelea hayatokei kwa bahati mbaya bali ni kutokana na uamuzi wa  chama hicho kuingia katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa na si ya kutafuta vyeo kama wengine walivyodhani hapo awali.

‘’Tulipoamua kuingia Serikalini si kwa kubahatisha, bali tulikuwa na ajenda zetu na ndio maana leo kila mmoja anaona mambo yameanza kubadilika’’alisema na kuongeza.

…Kila mmoja ni shahidi, jinsi Serikali ya Muungano  ikiongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan na kila mmoja ni shahidi jinsi mambo yanavyoendelea kubadilika.

 

Katika hatua nyengine, Othman ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais aliwataka wanachama wa ACT Wazalendo kujipanga zaidi kimageuzi na mabadiliko kwa kuwa ni sehemu ya dira ya chama hicho na hawana budi kukubali mabadiliko na kujianda. 

Kuhusu uwajibikaji kwa viongozi Serikalini, Othman alisema wanapaswa kufanyakazi kwa bidii zaidi wakitambua wamekula kiapo cha uaminifu hivyo wanapaswa muda wote kuonesha uwezo wao.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui amewataka wanachama kushikamana pamoja na kuunga mkono sensa ya watu na makaazi.

Amesema kushiriki kwao katika sensa kutaiwezesha Serikali kuwa na takwimu sahihi na kuweza kufanyakazi na pia chama kuandika Ilani ambayo itakidhi idadi halisi ya wananchi katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2025.

Mwisho

 

 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS