Header Ads Widget

DAWASA YACHUKUA HATUA YA KUJENGA MABWAWA YA KUTUNZA MAJI

 


KATIKA kukabiliana na changamoto ya upungufu wa maji inayoweza kujitokeza kipindi cha majira ya kiangazi Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imechukua hatua za kukabiliana na hali hiyo kwa kujenga mabwawa ya kutunza Maji.


Hayo yalisemwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge wakati wa ziara ya Wakuu wa Mikoa ya Pwani na Dar es Salaam Amos Makalla walipotembelea mitambo ya Ruvu Juu na Chini inayosukuma maji kupeleka maeneo mbalimbali ya Mikoa hiyo.


Kunenge alisema upatikanaji maji katika mto Ruvu ambacho ndicho chanzo kikuu kwa Mkoa wa Pwani na Dar es Salaam anawahakikishia wakazi wa Mikoa hiyo kuwa wameridhishwa na hali ya upatikanaji wa huduma.


"Pamoja na hali ya kiangazi kilichopo sasa wanachi wanapaswa kuchukua tahadhari mapema ili kudhibiti upotevu wa maji na tusijikute tunapambana na hali ya mwaka Jana,” alisema Kunenge.


Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla ameielekeza  Kamati ya Ulinzi na usalama na Mamlaka ya Bonde la Wami na Ruvu kufanya Operesheni za Mara kwa mara na kuwachukulia hatua watu watakaobainika kuchepusha maji bila Vibali.


Naye Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema Mamlaka hiyo inaendelea kufanya  kila jitihada za kuhakikisha kiasi Cha Maji kilichopo kinalindwa na kudhibiti upotevu na akawataka Wananchi  kutunza na kulinda Vyanzo vya Maji ili kuwepo na   upatikanaji wa maji ya uhakika.


Mwaka Jana maeneo mengi ya Jiji la Dar es salaam yalikumbwa na tatizo la uhaba wa maji Kutokana na ukame uliosababishwa na kutokunyesha kwa mvua za Vuli.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI