Header Ads Widget

BIL.145,162,500 ZAREJESHWA KATIKA VIKUNDI VYA VIJANA WAKINA MAMA NA WATU MWENYE ULEMAVU



**********

NA CHAUSIKU SAID, MWANZA.

Vikundi vilivyokuwa vimechukua fedha kinyume na taratibu, sheria na kanuni za fedha za mikopo ya asilimia 10 Mkoani Mwanza vimerejesha Bil. 145,162,500 katika mfuko wa vijana , wakina mama na watu wenye ulemavu.

Hayo yamebainishwa na Mkuuu wa Mkoa Mhandisi Robert Gabriel wakati akiwasilisha hali ya maendeleo ya mikopo ya asilimia 10 katika halmashauri zote za Mkoa huo.

Gabriel Amesema kuwa mnamo 25 April 2022 alitoa tamko kuhusu ukiukaji wa sheria,taratibu na kanuni za fedha hali iliyopelekea sh Bil.4.9 kutorejeshwa katika vikundi hivyo.

" kwa hiyo tumefanya hatua kubwa katika halmashauri zote kuhakikisha tuonaona fedha hizo zinarejea" Alisema Gabriel.

Amefafanua kuwa wakati ametoa agizo la kusimamisha zoezi la utoaji wa fedha kwa vikundi ndani ya miezi mitatu na kutaka fedha zote zilizokuwa zimechukuliwa kurudishwa na lengo la kufanya hivyo ni kutathimini na kuona watumishi ambao hawa kustahili kupewa mkopo hususani walioko kwenye ajira.

"Sasa fedha ni kwa ajili ya kuvisaidia vikundi anatokea mtu ameajiliwa anakuchukua fedha hizo na kusababisha walengwa hawafikiwi" Alisema Gabriel.

Gabriel amesema katika kuzuia zoezi hilo la utoaji fedha Halmashauri tayari zilikuwa zimetenga Bil.1,118,147, 483.16 kwa ajili ya kutoa kwenye vikundi.

Aidha ameeleza kuwa wakati wanapambana ili kuweza kurejesha madeni hayo fedha ambazo zilikuwepo ni takribani Million 209 ukijumuisha na pesa zilizorejeshwa baada ya kampeni hiyo sh Bil.145, 162, 500 ambapo jumla yake inakiwa Bil.1,254,542,750.

Gabriel amesema kuwa mpaka sasa kuna sh. Bil 2372690233.16 ambazo ziko tayari katika halmashauri zote kwa ajili ya kugawia vikundi vya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.

Aidha ametoa wito kwa vikundi vilivyohama Mkoani wa Mwanza kurudisha fedha walizokopa ili ziweze kusaidia vikundi vingine.

" Tunaomba warudishe fedha hizo kuna vikundi vimeitwa havijaitikia, tumevipa muda havijaonekana kuanzia wiki ijayo nitaitaji kukutana na vikundi vyote ambavyo hajijatekeleza majukumu ya marejesho ili tuweze kuzungumza navyo tutaanza na jiji la Mwanza kisha Manispaa ya Ilemela ili fedha zote zirudishwe ili ziingie kwenye mzunguko" Alisema Gabriel.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI