Na Fatma Ally Matukio Daima APP Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Liberata Mulamula amesema kumekuwa kumekuwepo na taarifa kubwa za upotoshaji kuhusu sakata la wananchi wa Loliondo kitu ambacho sio sahihi kwani kimekua kikileta sontofaham ndani na nje ya nchi.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam amesema kuwa, kuna clip (vipande vya video) ambavyo vimekua vikisambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu mauwaji yanayotokea Loliondo kwamba watu wanaoishi huko wanauliwa jambo ambalo sio sahihi.
"Watu wanachanganya kuna vitongoji viwili tofauti, Loliondo na Ngorongoro, watu Loliondo wanaondoka wenyewe kutokana na kuilewa dhamira ya Serikali juu yao ya kuwatafutia makazi sehemu ambayo ni salama kwao, na sio kama wanatolewa kwa nguvu kama watu wanavyopotosha"amesema Waziri Mulamula.
Amesema kuwa, kumekuwa na wanaharakati wanasambaza picha za uongo zikionesha watu wameuwawa kwa mapanga kinachoongelewa ni uongo wananchi wana uhitaji wa ardhi "amesema Mulamula.
Ameongeza kuwa, Serikali imekuja na mpango mkakati wa kuweza kuwatafutia maeneo mengine na wamepewa mazingira mazuri ya kuishi, nyumba nzuri na wanasafirishwa na mifugo yao.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Marry Masanja amesema kuwa taarifa zinazotolewa na baadhibya watu kuhusu Loliondo ni uongo kwani kuna kitalu ambacho amepewa mwekezaji kwa zaidi ya miaka 30, sasa kuupotosha umma kuwa wanahamisha watu Ili apewe muwekezaji.
"Taarifa inayosambazwa si ya kweli, kwa sababu muwekezaji aliyepo yupo muda mrefu na amekua akishindania na kushinda, watu wanaondoka kwa hiari yao na sio kama watu wanavyozusha, hali ni shuari hakuna ukweli zaidi ya huu tunaouweleza kwenu waandishi wa habari"amesema Naibu Waziri Massanja.
Aidha, amesema kuwa Katiba ya Tanzania inatambua haki ya binaadam ikiwemo kuishi hivyo hakuna mtu anayeondolewa kwa nguvu, wanaondoka wenyewe kutokana na kuona mazingira sio salama kwao wanakosa huduma za kijamii.
0 Comments