NA CHAUSIKU SAID MATUKIODAIMA APP MWANZA.
Jamii imetakiwa kutoendelea kuwaficha watoto wenye mahitaji maalum badala yake wawatoe hadharani na kuwapeleka shuleni ili waweze kujifunza na kuwa msaada katika jamii.
Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la BEYOND GIVING TANZANIA Joseph Msuka wakati akikabidhii Runinga yenye thamani ya sh 450, 000 katika shule ya Msingi Wita iliyopo kata ya kisesa Wilayani Magu yenye watoto wenye mahitaji maalum na kueleza kuwa jamii inapaswa kuwatambua watoto hao wanawajibu wa kupata elimu.
Msuka ameeleza kuwa kila mtu anawajibu wa kuhakikisha anamlinda mwenzie ili kuhakikisha kuwa watoto wenye ulemavu wanakenda shule, pia amefafanua kuwa Runinga aliyoitoa itawasaidia kujifunza watoto hao na kuongeza ufanisi katika masomo yao.
"Hii Runinga itawasaidia kujifunza mambo mablimbali ikiwemo kuangalia bunge na kuweza kupanua uelewa wao kwa kuona watoto wenzao katika hii Runinga namna wanavyovifunza" Alisema Msuka.
Msuka ameeleza kuwa kuna changamoto mbalimbali zinazowakumba watoto wenye ulemavu na wazazi wao ikiwemo umbali wa vituo vya kutolea elimu kwa watoto hao kushindwa kupelekwa shuleni ili waweze kupata elimu pamoja na mbiundombinu kutokuwa rafiki kwao.
" ukiangalia mtoto mwenye umri kuanzia 8-10 hauwezi kumbeba mgongoni kila siku kumpeleka shuleni kumtoa kijiji kimoja hadi kijiji kingine" Alisema Msuka.
Kwa upande wake Afisa Elimu kata ya kisesa Deogratias Lwanga ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo amesema kuwa Runinga hiyo itawsaidia walimu kufundishia n kuwaweka pamoja wanafunzi wenye mahitaji maalum na wasio na mahitaji maalum na kupunguza ubaguzi utapungua kabsa.
"Kwa sababu ukiangalia watoto wenye ulemavu kuna mazingira yanaweza kuwabagua lakini tukishakuwa na chombo kama hichi watoto watakuwa pamoja katika swala zima la elimu" Alisema Lwaga.
Ameeleza kuwa kutokana na vipaji alivyonavyo hivyo Runinga hiyo itawasaidia kukuza vipaji hivyo na kuviboresha zaidi.
Lwaga amewataka mashirika binafsi serikali kwa ujmla kuhakikisha watoto wenye ulemavu wanapata huduma staiki kama watoto wasio na ulemavu.
Said Joseph ni mkuu wa shule ya msingi Wita amefafanua kuwa bado kuna changamoto ya uhaba wa vifaa vya kufundishia kwa walimu wa vitengo hivyo vya watoto wenye ulemavu.
Said amewataka watu binafsi na mashirika kuendelea kuunga mkono jitihada za mashirika yanayojitolea kwa ajili ya watoto wenye mahitajiaalum.
Jaibi kazumari Ally mwalimu wa kitengo cha elimu Maalum ya Msingi Wita amesema kuwa kuna changamoto ya madarasa ambapo jumla ya wanafunzi 51wenye mahitaji maalum katika shule hiyo wasichina ni 21 na wavulana 20 na watoto wenye ulemavu wa kusikia na kuona wako madarasa matatu ambapo wanakaa darasa moja kuanzia darasa la kwanza hadi la tatu hali hali inayosababishwa na upungufu wa darasa.
"Inatulazimu sasa wanafunzi wote wanakaa darasa moja kuanzia darasa la kwanza hadi la tatu, wakati mwingine inatulazimu wengine watoke nje ili wengine waendelee kusoma" Alisema Ally.
Ally amefafanua kuwa changamoto hupekea kuwapa ugumu hususani wakati wa kufundisha ambapo walimu wawili hungia kufundisha kwa wakati mmoja huku kila mwalimu akiwa na ubao wake wa kufundisha darasa husika.
Lukia Rajabu ni mmoja wa wanafunzi wenye mahitaji maalum ameitaka jamii kutowaficha watoto wenye ulemavu ndani na wakakoswa masomo kama watoto wengine.
0 Comments