NA TITUS MWOMBEKI, Matukio Daima App Kagera.
Walimu wanaowafundisha watoto wenye mahitaji maalumu katika Shule ya Msingi Tumaini iliyopo kata Kashai Manispaa ya Bukoba wamesema kuwa wanakabiliwa na uhaba wa walimu wakusaidia kuwafundisha watoto wenye ulemavu katika Shule hiyo.
Hayo yamesemwa na mkuu wa kitengo cha watoto wenye mahitaji maalumu katika shule hiyo, John Mwita wakati wakizungumza na Matukio Daima baadaya kufika Shuleni hapo ambapo amesema kuwa katika shule hiyo kuna jumla ya walimu watatu ambao wanauwezo wa wakufundisha watoto hao huku akiomba waongezewe wengine watano ili kiweza kuongeza nguvu kazi ya ufundishaji watoto wenye mahitaji maalumu katika shule hiyo.
Wameongeza kuwa , Jumla ya toto (46) wenye ulemavu wa aina mbalimbali ukiwemo wa akili, usonji na viungo wamewekwa kwenye kitengo maalumu chakusoma katika shule hiyo.
"Watoto hawa kila mmoja ana mahitaji yake wawapo madarasani ili wapate kuelewa vizuri ni lazima wawepo walimu wa kutosha madarasani ili kuwasaidia kuwafundisha kwa ubora unaotakiwa kwani baadhi yao wanahitaji uangalizi mkubwa sana hasa wale wenye usonji make wakati mwingine huwa wanapatwa na hali ya kujidhuru hususani akipata kifaa nyenye ncha kali na kwa sisi tulioko hapa tunaingia mwalimu mmoja mmoja kwa kila hatua maana zipo hatua tatu kuanzia ya kwanza mpaka ya tatu"
" kulingana na mpangilio wa madarasa kikawaida wastani kwa walimu kufundisha wa toto wa namna hii huwa ni mwalimu mmoja kwa mtoto mmoja hasa hawa wenye usonji pamoja na mwalimu mmoja kwa wanafunzi wanne wa ulemavu wakawaida lakini sisi hapa tunalazimika kuwachanganya pamoja wakati wa masomo darasani yote hiyo ni kutokana na uchache wetu tuliopo hapa" ameeleza Mwita.
Pia wameishukuru Serikali kwa jitihada za kuweka miundombinu wezeshi ya kuwasaidia katika ufundishaji pamoja na chakula kwa kila siku wawapo shuleni watoto hao hula kabla ya kurudi makwao , hivyo wameiomba kuendelea kuwasaidia kwani bado kuna mahitaji mengine kama vile viwanja vya michezo, bembea, chumba maalumu cha kuwasaidia kuwahudumia watoto hao pale wanapokutwa na matatizo ya kiafya kulingana na ulemavu wao.
Mweka hazina wa chama cha watu wasioona Mkoa Kagera, Deogratias Kato amewatia moyo walimu hao kuwa kutokana na changamoto wanazokumbana nazo katika kutekeleza majukumu yao huku akiiomba serikali kuzidi kukaza kamba katika kuhakikisha inazitatua changamoto hizo kwa ukaribu ikiwemo ya kuongeza walimu maalumu katika vituo vya kufundishia watoto wenye mahitaji maalumu hali itakayosaidia watoto hao kupata elimu ipasavyo.
0 Comments