Header Ads Widget

WALIMU WAKAMATWA KWA TUHUMA ZA KUKUTWA NA VIUNGO VYA BINADAMU


Kamanda wa polisi mkoa Kigoma James Manyama (wa pili kushoto) akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini Kigoma.

 

Jeshi la polisi mkoa Kigoma limebaini viungo vya binadamu vilivyokamatwa Mkoani humo Juni 3,2022 ni viungo vya Bilihanyuma Suminda, mzee mwenye miaka 90 ambaye alizikwa mwezi Januari mwaka huu


Akitoa muendelezo wa taarifa ya watu waliokamatwa na viungo vya binadamu Juni 3 mwaka huu Kamanda wa polisi mkoa Kigoma, James Manyama  amesema kuwa polisi wamefukua kaburi la mtu ambaye viungo hivyo vilifukuliwa na kuthibitisha kuwa vilikuwa ni viungo vya Bilihanyuma Suminda, mzee mwenye miaka 90 ambaye alizikwa mwezi Januari mwaka huu.

Kamanda huyo wa polisi amewataja watuhumiwa hao akiwemo Bankana Zakayo (41) aliyekuwa Sengerema mkoa Mwanza ambaye alikuwa akipelekewa viungo hivyo na Miraji Nyambi (45) aliyekuwa dereva wa gari lililokamatwa na viungo hivyo ambao wote ni walimu wa shule ya sekondari Mwandiga wilaya ya Kigoma.

Sambamba na hao  amewataja pia Mathayo Ndayishimiye (40) Mganga wa kienyeji kutoka nchini Burundi, Ramadhani Abrahaman (52) Mganga wa kienyeji, Adizino John (62), Nguno Manyanza (49), James Kibeba (68), Kelvin Fedha na Thobias Fundo (33).

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI