Header Ads Widget

WAKULIMA WA PARACHICHI NJOMBE WATIWA MOYO.



Na Gabriel Kilamlya NJOMBE


Hofu imetolewa kwa wakulima wa parachichi mkoani Njombe kuacha kukata tamaa kutokana mdororo wa soko la tunda hilo na kwamba soko la tunda hilo limeanza kufunguka taratibu na hivyo wakulima hawapaswi kuacha kulima.


Hii inakuja baada ya kuwapo kwa mkwamo mkubwa wa parachichi sokoni sababu zikitajwa ni kutokana na vita vya ukraine na Urusi ambako kulikuwa na masoko makubwa ya tunda hilo,vita vilivyosababisha wakulima wengi na makampuni ya ununuzi wa tunda hilo kupata hasara kubwa.



Miongoni mwa makampuni yaliyoingia kwenye mkwamo huo ni pamoja na kampuni ya kizawa ya shikamoo parachichi ya mkoani njombe chini ya mkurugenzi wake Erasto Ngole ambayo mbali na changamoto za kibiashara lakini ilijikuta inashindwa kununua matunda hayo kwa wakulima ambao baadhi yao walionekana kukata tamaa.


Ngole pia anakiri kuwa mkwamo huo ulisababisha kampuni yake kudaiwa na  wakulima takribani shilingi milioni 40 ambazo hata hivyo  zimeshalipwa na zoezi la ununuzi wa matunda hayo linaendelea.


Nimelazimika kuwatafuta baadhi ya wakulima waliokuwa wanafanya kazi na kampuni hiyo ili kujua kama ni kweli wamelipwa fedha hizo ambapo Petro Luganga,Emmanuel Msigwa na Joseph Kabelege toka Matembwe wanakiri kulipwa fedha zao licha ya mkwamo uliotokea.


Kwa mujibu wa soko la parachichi aina ya hasi hivi sasa kilo moja baadhi ya wanunuzi wananunua shilingi elfu 1200 hadi 1250.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS