Header Ads Widget

TMDA SASA KUDHIBITI TUMBATU, SHISHA

 


Na Mwandishi wetu, Mtwara


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Masasi Elias Ntiruhungwa ameipongeza Wizara ya Afya  kwa kutoa jukumu kwa Mamlaka ya Dawa na VifaaTiba (TMDA) la kudhibiti bidhaa zinazotokana na mazao ya Tumbaku hapa nchini ambapo kwa sasa  ni sigara,shisha.


Kauli hiyo ameitoa jana katika kikao kazi cha  wafamasia wa halmashauri za Mkoa wa Mtwara, kilichofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi ambapo alisema kuwa matumizi ya bidhaa hizo yamekuwa yakiongezeka hali ambayo inaweza kuleta madhara makubwa kwa jamii. 


Alisema kuwa taasisi inatambua mchango mkubwa wa wakaguzi na wataalamu waliopo katika ngazi za Mikoa na Halmashauri kutoka TMDA.


“Hawa TMDA wanajukumu kubwa la Kufanya ukaguzi na ufuatiliaji wa bidhaa kwa kudhibiti utengenezaji, uingizaji na usambazaji wake ikiwemo kufanya uchunguzi wa kimaabara ili kuhakikisha kuwa bidhaa husika zina fikia viwango vya ubora na usalama”


Pia wanalo jukumu kubwa la Kuelimisha jamii kuhusu ubora, usalama na matumizi sahihi ya dawa, vifaa tiba&vitendanishi ikiwemo na Kudhibiti uingizaji na utoaji nje ya nchi wa bidhaa ikiwa ni pamoja na dawa za kulevya, Kufuatilia madhara yatokanayo na matumizi ya dawa, vifaa tiba&vitendanishi sambamba na kuteketeza bidhaa duni na bandia” 


Kwa upande wake Meneja TMDA Kanda ya Kusini, Dkt. Engelbert Bilashoboka Mbekenga, alisema kuwa wakaguzi  wanapaswa kuwa watiifu katika kazi zao kwani kazi yao ni ngumu na inahitaji utiifu katika kulinda afya ya jamii.


“Lengo mahususi la Kikao kazi hiki ni kukumbushana kazi ambazo zinafanywa na TMDA, ambazo wamekasimishwa Halmashauri katika kusaidia kufanyakazi hizo kwa weledi, kazi hizo ni kufanya ukaguzi kwenye maeneo yanayotoa huduma za afya kama maduka ya dawa, maabara, zahanati, vituo vya afya na hospitali lengo likiwa ni kuangalia usalama, ubora na ufanisi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi kwa upande wabinadamu na mifugo” alisema Bilashoboka


mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS