NA HADIJA OMARY, MatukioDaimaAPP,Lindi
Mkuu wa wilaya ya kilwa mkoani Lindi Bi. Zainab Kawawa amewataka vijana wilayani humo kutumia fulsa za uwepo wa vivutio vya utalii katika Wilaya yao kujinufaisha kiuchumi
Kawawa ameyaseama hayo wakati wa tamasha la kuhamasisha utalii wa ndani na kutembelea hifadhi ya Msitu wa pindiro Uliopo Wilayani humo wenye vivutio mbali mbali ikiwemo viboko Albino ambao hawapatikani sehemu yoyote ya hifadhi hapa Nchini.
Tamasha hilo lililowakutanisha vijana kutoka katika halmashauri mbali mbali za Mkoa wa Lindi na Mtwara liliandaliwa na Wakala wa Mistu Tanzania (TFS) lilikuwa na lengo la kuunga Mkono jitiada za Rais Samia Suluhu Hassan katika kutangaza vivutio vya utalii hapa Nchini ikiwa ni miezi michache baada ya kuzinduliwa kwa Filam ya Royal Tour
Bi. Zainab alisema kuwa uwepo wa vivuti vilivyopo katika Wilaya hiyo ni fursa tosha kwa vijana kujinufaisha kiuchumi kwa kutengeneza vitu mbali mbali vya kisanaa vitakavyowavutia wageni wanaotembelea katika maeneo hayo kununua.
“kawaida wageni wanapokuja kwenye vivutio hivi vya utalii , watakuja kuviona vivutio hivi lakini pia watapenda kuondoka na Zawadi na kumbu kumbu , sasa zawadi hizo wakuzitengeneza ni sisi vijana kwa hivyo tuone uwepo wa vivutio hivi ni fursa kwetu” alisema Kawawa
Kawawa aliongeza kuwa Kitendo cha Rais Samia kuzindua Royal tour kumefungua njia ya kuleta ajira kwa vijana hivyo ni muhimu kwa vijana hao kuunga jitihada hizo kwa vitendo ili kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
Awali mhifadhi Mkuu wa Wakala wa Mistu Tanzania TFS Bw. Abbas Said alieleza kuwa upekee wa msitu huo wa hifadhi ya Pindiro ni uwepo wa Boko ambao hawapatikani eneo lolote hapa Nchini Tanzania ambao uwa wanatabia ya kuhama kutoka sehemu wanayoishi kwenda Mto Mbwenkuru kipindi cha masika
“wataalamu wanasema kitendo cha boko hao kuondoka kipindi cha masika ni kwa sababu ya kuzaliana , pamoja na boko pia wapo Wanyama mbali mbali kama vile mamba ndege na wengine”
Alisema kutokana na upekee wake wanavyuo wengi wamekuwa wakifika kwa ajili ya kufanya tafiti mbali mbali zinazohusu maswala ya ikolojia.
Hata hivyo Abbas alisema kuwa pamoja na upekee wa boko hao Albino waliopo ndani ya Msitu huo lakini uwenda boko hao wakatoweka kutokana na shughuli za uwindaji zinazofanywa na baadhi ya wananchi.
Kwa upande wake Rahma Kipangala mdau wa Utalii Wilayani Kilwa Mkoani Lindi ameiomba Serikali kuboresha miundombinu ya barabara inayokwenda katika msitu huo wa pindiro ili kuwawezesha watalii kufika katika hifadhi hizo kwa urahisi.
0 Comments