Na Gabriel Kilamlya ,Matukio DaimaAPP NJOMBE
Wakati chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Njombe kikitarajia kuanza zoezi la uchaguzi mkuu wa ndani hapo julai 2 mwaka huu kwa ngazi ya wilaya na Mkoa onyo kali limetolewa kwa baadhi ya wanachama wenye tabia ya kuwachafua wengine na kutumia rushwa kupata madaraka.
Kauli ya chama hicho chini ya katibu wa siasa na uenezi ccm mkoa wa Njombe Erasto Ngole inakuja baada ya kutangazwa kwa mchakato huo ambao unatarajia kuanza julai 2 hadi 10 katika nafasi za Uenyekiti,Uenezi,ujumbe pamoja na jumuiya za vijana,wanawake na Wazazi katika ngazi ya Wilaya na Mkoa.
Aidha Ngole anasema Chama hicho kimejipanga vyema kudhibiti changamoto hiyo pindi itakapojitokeza na hakiko tayari kuruhusu hayo.
Khamis Ally Kachinga ni katibu wa jumuiya ya vijana ccm mkoa wa Njombe ambaye anawataka vijana kutumia fursa hiyo katika kuomba kugombea nafasi mbalimbali ili walisaidie taifa katika kujiletea maendeleo Huku katibu wa jumuiya ya wazazi Mkoa Bi.Agatha Lubuva akikemea vitendo vya rushwa wakati wa uchaguzi huo.
Vijana ndio wanatajwa kutakiwa kujitokeza kwa wingi kugombea katika nafasi mbalimbali za uongozi ambapo baadhi yao akiwemo Johnson Mgimba wanasema hawatokuwa nyuma katika mchakato huo.
Noel Mseo ni naibu mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU Mkoa wa Njombe ambaye anasema tayari wameanza kuchukua hatua mbalimbali za kufuatilia mchakato huo pamoja na kutoa elimu kwa wanasiasa wenyewe.
Uchaguzi huo unakuja baada ya viongozi wake kuhudumu katika kipindi cha miaka mitano baada ya kuchaguliwa mwaka 2017.
0 Comments