Header Ads Widget

VIJANA WAPATIWA MAFUNZO KUDHIBITI MIGONGANO BAINA YA TEMBO NA BINAADAMU

 


Na HADIJA OMARY, LINDI.


MKUU  wa wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi Hashimu Komba ameipongeza Serikali kwa Jitihada inayoendelea kuzifanya ili kuhakikisha inamaliza changamoto za Wanyama wahalibifu aina ya Tembo katika Wilaya yao.


Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Katibu Tawala Wilaya ya Nachingwea Omary Mwanga wakati wa mafunzo ya namna ya kudhibiti Migongano  baina ya Binaadamu na Wanyama Pori kwa vijana 60 kutoka katika kata saba zilizoathilika na Wanyama hao wahalibifu aina ya Tembo alisema  wanaishukuru Serikali kwa namna  inavyochukua hatua katika kuwaondoa Wanyama hao.



Mwanga alisema Wanyama hao wahalibifu wamekuwa wakileta athari katika baadhi ya Maeneo Wilayani humo  hasa kwa nyakati hizi za kiangazi kwa  kuharibu mazao ya wakulima na kusababisha wanachi kukosa chakula.


Hata hivyo mwanga pia alitumia fulsa hiyo kuwataka washiriki wa Mafunzo kuyazingatia kikamilifu mafunzo  hayo ili yawe na faida kwao pamoja na kuweza kusabaza elimu hiyo kwa jamii inayowazunguka.



“swala la kudhibiti Wanyama pori lisiwe ni swala letu pekeetu sisi washiriki tuliopewa mafunzo, tunatamani Elimu hii waipate hat ana wenzetu ambao hawakupata wasaha wa kufika hapa, ili linapokuja ilo swala tuweze kushirikiana kwa pamoja kuweza kuwadhibiti Wanyama hao” alieleza Mwanga.


“Changamoto hii ya Wanyama wahalibifu sio ya Wilaya ya Nachingwea peke yake hivyo sisi kupata fulsa ya Wataalamu hao kufika katika Wilaya yetu na kutoa Mafunzo tuone hili ni jambo hadhimu sana lakini pia tuone ni kwa namna ya Serikali kwa Dhati kabisa kuhakikisha inataka kuondoa changamoto hii kwenye Wilaya yetu”


Kwa upande wake Mtafiti kutoka Taasisi ya Utafiti Wanyama Pori (TAWIRI) DKT. Emanuel Masenga alisema kuwa katika Warsha hiyo Washiriki watafundishwa namna ya kutumia vifaa mbali mbali ambavyo vinatumika kuwaondoa tembo anapoingia kwenye makazi ya watu pamoja na mbinu za kuzuia Wanyama hao wasiingie kwenye makazi ya watu.



“kwa muitikio huo tunaona wanafunzi waliochaguliwa wataenda kuwa mabalozi wazuri katika vijiji husika kwa kuunda vikundi Shirikishi vya kukabiliana na Wanyama hao wakali aina ya Tembo”


Kwa upande wake Afisa Wanyama pori kutoka  Mamlaka ya usimamizi wa Wanyama pori Tanzania (TAWA) Frenk Mapunda Alisema kuwa baada ya kutambaua maeneo na mtawanyiko wa Tembo waliovamia katika Mashamba ya Wananchi na kuendelea kuwafukuza kurudi katika Maeneo ya Hifadhi wamekutana na changamoto ya uwepo wa makundi makubwa ya Tembo kwenye misitu iliyopo kwenye vijiji.



Nae Diwani wa kata ya Namapwia Omary Lingumbende , Licha ya kuishukuru Serikali kwa namna walivyolipa uzito swala hilo la kuwaondoa Wanyama hao katika maeneo yao kwa kuleta vikosi kazi vya kuwarudisha Tembo hao hifadhini  pamoja na kutoa mafunzo kwa vijana kwa ajili ya kushirikiana na kikosi kazi hiko pia ameiomba Serikali kupeleka fidia kwa wananchi walioathilika ili waweze kuokoka na janga la Njaa.


MWISHO

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI