Header Ads Widget

SHEKH ALHAJ MUSTAPH SHABANI "WALIMU WA DINI FUNDISHENI MAADILI".



NA HAMIDA RAMADHAN DODOMA


WALIMU wa dini nchini wametakiwa kuhakikisha wanafundisha maadili kwa wanafunzi ili kukikomboa kizazi cha leo na chakesho kwani shuhuda zinaonesha Mmomonyoko wamaadili umefikia katika hali ya kukatisha tamaa.


Shekh wa Mkoa wa Dodoma,Alhaj Mustaph Shabani aliyasema hayo jijini hapa katika Warsha ilioandaliwa na viongozi wa Islamic Education Panel lengo likiwa ni kuhimiza maadili kwa wanafunzi ambapo ameeleza hatari zaidi ni pale inapofikia jamii kuaanza kukubali mmonyoko kuwa sehemu ya kawaida ya maisha ya kila siku.



Alisema uhalimu ni wito warsha hii iwe endelevu na ikiwezekana ipangiwe siku Maalum kila mwaka au kila baada ya miezi kadhaa ili walimu wapate jukwaa Kama hiki la kusemea. 


"Niukweli kwamba jamii haiwezi kutengamaa wala demokrasia haiwezi kusimama bila ya kuwa na vikao Kama hivi vya kuwakkunusha Walimu juu ya malezi kwa watoto" Alisema Shekh Mustaph.


Aidha  Shekhe Mustaph alisema ,zipo nyakati namatukio ambayo baadhi ya wale waliobeba jukumu lakulea,nao wamekuwa sehemu ya waharibifu huo.


"Matukio yote maovu kwa vijana wetu yanatukumbusha kuwa bado tuna kazi na wajibu mkubwa mbele yetu kwakutimiza wajibu na kujua nani anabeba dhima ya ujenzi au kubomoa maadili ya jamiili na kuwepo kwa mjadala mpana kwa wanachuoni," alisema Shekhe Mustaph


Hata hivyo alisema inafahamika kuwa mwalimu anaongozwa na mtaala katika kutekeleza sehemu kubwa ya majukumu yake kwaupande mmoja inawezekana mtaala haujasema kwamapana sehemu ya malezi,na kwaupande mwinguine mtaala wa walimu waelimu unalalamikiwa kuwa nachangamoto kadhaa katika kukidhi mahitaji ya jamii ya sasa," alisema Shekhe Mustaph


Kwa Upande wake Afisa Elimu wa jiji la Dodoma idara ya sekondari Mwl Upendo Rweymamu alipokuwa akimuwakilisha Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Joseph Mafuru alisema katika kwa pamoja tunawajibu wadhati wa kutumia akili na nguvu alizotupa Mwenyezi Mungu kuweka jitihada katika kutekeleza majukumu yetu bila kuathiriwa na changamoto zilizopo.


Alisema miongoni mwa vipimo sahihi vya kumpima mwalimu ni kuiangalia jamii anayoihudumia hii ni kwasababu tumeona kuwa mwalimu ndiye muundaji wa mtu mmoja mmoja na hatimaye jamii nzima.


Alieleza Mazuri ya nayofanyika katika jamii ni tafsiri ya mafanikio ya kazi ya mwalimu halikadhalika, mabaya yote yanayofanywa na jamii ni ishara ya kutofanikiwa kwa kazi ya mwalimu.


Pia alisema Serikali imeweka vipindi vya Dini kila wiki kwenye shule zetu za msingi na sekondari hali kadhalika imetoa mwongozo wakupata walimu wakufundisha vipindi hivi vya dini Mwongozo huo unaowataka walimu wa kuu shule kupata walimu wakufundisha masomo ya dini


KUHUSU WANAFUNZI WANAOSO MASOMO YA DINI


Aidha alisema bado wanafunzi wanaosoma masomo ya dini na kutahiniwa ni wachache ambapo wachache wanaosoma na kutahiniwa ufaulu wao badoniduni.


"Hali hii inaashiria nguvu hafifu ya

walimu kwenye eneo hilo Ikiwa hatua za makusudi hazita chukuliwa na walimu,taifa litazama kwenye dimbwi la maovu na uhalifu," amesema 


Na nakuongeza"Tafa letu limeanza kushuhudia athari za moja kwa moja za watoto wetu kutokulelewa katika maadili mema Kesi zapanyarodi, matumizi ya dawazakulevya, ngono na mimba kwa wanafunzi ni miongoni mwa mambo ya nayoanza kuzoeleka kwenye masikio ya watanzania,"alisema Afisa huyo.



Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI