Header Ads Widget

JAJI MKUU PROF. IBRAHIM JUMA AWAKUMBUSHA MA-RC NA DC KUZIKUMBUKA MAHAKAMA.



 Na Mwandishi wetu, Mtwara


JAJI Mkuu wa Mahakama Nchini Profesa Ibrahim Juma awakumbusha  Wakuu wa mikoa na Wilaya kuwa na utamaduni wa kuikumbuka na kuwajumuisha Mahakama katika Mambo ya maendeleo ikiwemo umeme, makazi na mkongo wa Taifa. 


ombi hilo amelitoa Jana wakati akizungumza na wenyeviti wa kamati za mikoa, wenyeviti wa kamati za maadili Wilaya na wajumbe wa kamati hizo katika kutoka mkoa wa Mtwara ambapo alisema kuwa mahakama unapaswa kukumbukwa. 


"Unajua mahakama zipo kwenye maeneo yetu zinapaswa kukumbukwa kwenye maendeleo hasa kwenye miradi inayoletwa na serikali 

Wakuu hao wa mikoa na Wilaya kuhakikisha na Mahakama shughuli za maendeleo zinapofika kwenye vijiji ziwe zinafika pia kwenye mahakama" 


"Mfano Tanecso ukiwa na mradi wa umeme vijijini msisahau umeme Mahakama za mwanzo, ambazo ziko karibu zaidi na wananchi  tumezisogeza ili wananchi waweze kupata huduma kwa ukaribu japo watumishi wetu wanaishi katika mazingira duni 


Alisema kuwa usogezwaji wa huduma unaweza kuchangia maboresho makubwa katika mahakama ambapo  anuani za makazi zimeonyesha kuwa na umuhimu zaidi. 


Kwenye Anuani za makazi msisahau mahakama kwakuwa zinawaongoza kujua wanaoleta mashauri, wanaopewa dhamana mazingira wanayotokea kwa itabidi zaidi" Alisema Jaji Juma


Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brigedia Generali Marco Gaguti alisema kuwa ni muhimu mahakama zikawepo kwenye miji midogo inayoanzishwa kutokana na umuhimu wa huduma zinazotolewa na chombo hicho. 


"Mfano hapa ipo miji mipya inaanzishwa ni muhimu mahakama za mwanzo zitaanzishwa msimamo  nitaisimamia ili kuhakikisha maeneo ya mahakama yanaanzishwa  na makazi ya watumishi yanatengwa ili kuhakikisha kuwa wanapata mazingira" alisema Gaguti


MWISHO

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI