Na Matukio Daima Media, Iringa
Aliyekuwa mgombea wa ubunge Jimbo la Kalenga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Grace Tendega, amesema kuwa licha ya kutoshinda katika kura za maoni, ataendelea kuwa mwanachama mwaminifu wa chama hicho na kushiriki kikamilifu katika kampeni za kuwanadi wagombea wa CCM kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba.
Tendega, ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), alishika nafasi ya pili kati ya wagombea wanne waliowania kupitishwa kugombea ubunge kupitia CCM, ambapo alipata kura 2,391.
Mgombea aliyeshinda Jackson Kiswaga, alipata kura 4,036 akizungumza mara baada ya kuchukua matokeo katika ofisi za CCM Wilaya ya Iringa Vijijini, Tendega alisema kuwa kushindwa ni sehemu ya mchakato wa kidemokrasia, na haipaswi kuwa sababu ya mtu kukihama chama.
> "Kwa mchakato huu, naona wazi kuwa wanachama na chama kwa ujumla wananitambua na kuniunga mkono Nitabaki ndani ya CCM kuendelea kufanya kazi za chama na kuhakikisha mgombea atakayeteuliwa anapata ushindi mkubwa," alisema.
Aidha, aliwahimiza wanachama waliokosa nafasi ya kupitishwa katika kura za maoni kutokata tamaa wala kuhama chama, bali waendelee kujenga umoja na mshikamano ndani ya CCM.
> "kugombea ni mchakato Ukikosa unashukuru, ukipata unashukuru Mwenyezi Mungu ndiye hutoa uongozi hivyo, sina mpango wa kufanya chochote nje ya chama hiki," alisisitiza.
Tendega aliushukuru uongozi wa CCM kwa kumpatia nafasi ya kushiriki mchakato huo, akisema kuwa hii ni mara yake ya kwanza kugombea nafasi ya ubunge kupitia CCM.
> "Nawashukuru sana wanachama na wananchi wa Jimbo la Kalenga kwa kuniamini hii ni hatua kubwa na mwanzo mzuri kwa safari yangu ndani ya chama hiki Oktoba tutakwenda kutiki kwa juhudi kubwa kuhakikisha ushindi kwa rais, wabunge na madiwani wa CCM," aliongeza.
Huku mgombea aloyeongoza mchakato huo Jackson Kiswaga akiwashukuru wagombea wenzake pia kushukuru wajumbe kwa kumuamini tena na kuwa jina likirejea na akishinda ubunge atawatumikia vema wananchi wa Kalenga
Katika mchakato huo wa kura za maoni, wagombea walioshiriki na matokeo yao ni kama ni pamoja na mbunge aliyemaliza muda wake Jackson Kiswaga – kura 4,036,Grace Tendega – kura 2,391,Musa Mdede – kura 1,281,Henry Nyaulingo – kura 304
0 Comments