Header Ads Widget

SERIKALI IMEOMBWA KUJENGA KITUO CHA POLISI KATA YA IHANGA MKOANI NJOMBE.



Na Gabriel Kilamlya NJOMBE


Kufuatia kushamiri kwa vitendo vya Mauaji vinavyotokana na migogoro ya Ardhi pamoja na imani za kishirikina kwa Wananchi wa kijiji cha Ihanga mkoani Njombe  serikali imeombwa kujenga kituo cha Polisi katika Kata ya Ihanga ili kukomesha vitendo hivyo.


Wananchi wa vijiji vya Kata ya Ihanga kwa nyakati tofauti wamewasilisha maombi hayo kwa Mkuu wa wilaya ya Njombe Kisa Kasongwa akiwa ziarani katika Kata hiyo akiwa ameambatana na kamati ya Ulinzi na Usalama kusikiliza kero za Wananchi ambapo pia katika Kijiji cha Itipula imeelezwa kuwa Mwananchi mmoja amevamia eneo la Shule ya Msingi na   Eneo la kijiji zaidi ya Ekari 27.



Wananchi wa kijiji cha Ihanga akiwemo Kasiani Kigora na Theofili Mwinuka ambaye ni Afisa Mtendaji wa Kata ya Ihanga wanakiri kuwapo kwa mauaji ya mara kwa mara yanayotokana na migogoro ya Ardhi.


Mwakilishi wa Mkuu wa Polisi wilaya ya Njombe Mkaguzi wa Jeshi la Polisi Magreth Mbawa amesema kuwa kata hiyo imekuwa tishio kwa mauaji kutokana na migogro ya Ardhi pamoja na imani za kishirikina huku akiwataka kuacha vitendo hivyo mara moja.



Awali Katibu Tawala wilaya ya Njombe Emmanuel George ameagiza wauzaji na wanunuzi wa Ardhi kufuata sheria huku Mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa akiagiza Viongozi wa Vijiji vya Kata hiyo kuorodhesha majina ya Wananchi walio vinara wa migogoro ya Ardhi ili kamati ya Ulinzi na Usalama iyafanyie kazi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI