Header Ads Widget

MHAKAMA YATOA SIKU 14 UPELELEZI KESI YA SABAYA KUKAMILIKA.

 


NA WILLIUM PAUL, MOSHI.

 

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi mjini Moshi mkoani Kilimanjaro imetoa siku kumi na nne kwa upande wa Jamuhuri kuhakikisha unakamilisha upelelezi katika kesi ya Uhujumu Uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wanne.

 

Akieleza maamuzi hayo, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Salome Mshasha alisema kuwa, katika kumbukumbu za mahakama siku ya kwanza kufikishwa kesi hiyo mahakamani hapo upande wa Mwendesha mashitaka wa Serikali alipokuwa akiwasomea washitakiwa maelezo ya awali ambapo hawakutakiwa kujibu chochote alisema upelelezi umekamilika.

 


Alisema kuwa, kwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza shauri hilo walipaswa kusubiri kibali cha Mwendesha mashitaka mkuu wa Serikali (DPP), kama ataridhia mahakama hiyo kusikiliza ambapo siku iliyofwata na jana pia upende wa Jamuhuri umedai kuwa upelelezi haujakamilika tena.

 

“Nimesikiliza maelezo ya pande zote mbili na nimeona hoja za upande wa utetezi na kuona ni za msingi kwamba siku ya kwanza Jamuhuri walisema upelelezi umekamilika lakini siku ya pili na leo ya tatu wanasema upelezi haujakamilika hivyo mahakama inatoa siku kumi na nne kuhakikisha upande wa Jamuhuri unakamilisha upelelezi ili washitakiwa wapate haki yao” alisema Salome.

 


Awali kabla ya maamuzi hayo upande wa Jamuhuri ukiongozwa na Wakili  wa Serikali Mwandamizi, Veridiana Mleza alisema kuwa, kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutajwa ambapo upelelezi haujakamilika na pia faili limeshakwenda wa DPP kwa ajili ya kusainiwa ili kuipa haki mahakama hiyo kusikiliza hivyo aliomba kupangiwa tarehe nyingine ya kutajwa.

 

Upande wa utetezi ukiongozwa na Wakili Hellen Mahuna alisema kuwa, hawana pingamizi kuahirishwa kwa kesi lakini wanayo malalamiko machache ambapo upande wa Jamuhuri siku ya kwanza walisema upelelezi umekamilika lakini siku ya pili na jana wamesema upepelezi haujakamilika.

 

Hellen alisema kuwa, upande wa Jamuhuri haupo siriasi kukamilisha upelelezi kwani watuhumiwa wanateseka na kama alivyosema awali Mstitakiwa wa kwanza (Sabaya) ni mgonjwa hivyo aliiomba mahakama hiyo kuisukuma Jamuhuri kukamilisha upelelezi haraka na kibali kutoka kwa DPP ili kesi hiyo iweze kuendelea.

 


SABAYA AFUNGUKA MAHAKAMANI.

Naye  Sabaya alisema kuwa, kesi hiyo ililetwa mara ya kwanza na alilalamika kesi hiyo ni ya kuonewa na alimlalamikia aliyekuwa Wakili wa Serikali Tumain Kweka na kumuomba Mwendesha mashitaka mkuu wa Serikali kutambua kinachoendelea katika ofisi yake ni uonevu.

 

Alisema kuwa, yeye anaumwa na huko anapoenda ni magereza na sio eneo la starehe (pikiniki), na kudaikuwa mashitaka yanayopokelewa katika ofosi ya DPP na hasa Takukuru ni ya kiuonevu na yanatengenezwa.

 

Kesi hiyo imepangwa kutajwa tena Julai 4 mwaka huu ambapo watuhumiwa wote wamerudishwa mahabusu.

 

Katika kesi hiyo washitakiwa ni Lengai Ole Sabaya, Silvester Nyegu, John Aweyo, Nathan Msuya pamoja na Antero Assey ambapo wanakibiliwa na makosa saba likiwemo la utakatishaji fedha.

 

Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI