Na Hamida Ramadhan Matukio Daima App, Dodoma
MRATIBU na Muwakilishi wa Shirika la Mazingira kutoka Umoja wa Mataifa Clara Makenya amesema matatizo matatu yanayoikumba duniani nipamoja na mabadiliko ya tabianchi, uharibifu wa baioanuai na uchafuzi wa hali ya hewa.
Mratibu huyo alisema hayo Jijini hapa wakati akizungumza na waandishi was habari katika wiki ya Mazingira iliyomalizika jana ambapo alibainisha kuwa Shirika la Mazingira la umoja wa mataifa (UNEP) kwa kushirikiana na mashirika mengine saba wamekuwa wakichukua hatua mbalimbali kukabiliana nayo ambayo
Aidha, alisema wanaangalia namna wanavyoshirikiana na serikali kukabiliana na hali hiyo kwa kuhamasisha matumizi ya nishati mbadala kupunguza mabadiliko ya tabia nchi na athari za majanga.
Vilevile, alibanisha vipengele saba vinavyozingatiwa kukabiliana na hali hiyo ambavyo ni kuwezesha kuwepo kwa takwimu zifakazotoa ushauri ili kuwepo usahihi kwa wafanya maamuzi.
Vipengele vingine ni uwepo wa sera itakayoelekeza wadau namna Tanzania itakavyokabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, teknolojia kupunguza uharibifu.
Aidha,kuwepo utafiti ili kutoa taarifa zinazoelekeza upande gani una changamoto ili hatua zichukuliwe kukabiliana na hali hiyo na kuwepo ushirikiano na wadau mbalimbali, mashirika yasiyo ya kiserikali na jamii kwa ujumla.
"Tunahakikisha kila eneo lina kipengele kinachosaidia kukabiliana na changamoto hizo tatu za mazingira zinazoikabili Dunia,"alisema Clara.
Kwa Upande Muwakilishi kutoka wizara ya Nishati mbadala Emilian Nyanda alisema watahkikisha wananchi wanatumia nishati mbadala kwa lengo la kutunza mazingira kwani Wizara ya Nishati imekuwa ikihamasisha jamii juu utumiaji wa Nishati mbadala na kuondokana na Nishati ambazo Zina madhara kwa jamii.
alisema Wizara kwa kushirikiana na Umoja wa ulaya wameanzisha mradi wa Nishati ya kupikia uliogharimu takribani uro milion 30.
"Mradi huu utakuwa ukisaidia mashirika binafsi na unatekelezwa katika mikoa 5 ambayo ni dodoma, Daresalam, Mwanza, morogoro na pwani huku akibainisha kuwa Wizara itaendelea kuhamasisha jamii kutumia Nishati mbadala," Nyanda.
Naye Mratibu wa Mradi unaochangia kuzuia athari za mabadiliko ya tabianchi, Aine Mushi alisema shirika hilo limekuwa likihamasisha kuhusu matumizi ya Nishati mbadala na wameanzisha mradi wa kuweka Nishati hiyo katika wilaya ya Chamwino, Kondoa, Mpwapwa.
"Lengo la mradi huu ni kuonyesha na kuweka Nishati mbadala na kuelekea kuhusu matumizi ya mkaa mbadala hasa katika maeneo ambayo tunaweza kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi," alieleza.
Pia, alisema wanahamasisha kuhusu matumizi ya nishati mbadala ili Sera zinazosimamia zitekekezeke katika nyanja za kimataifa.
0 Comments