Header Ads Widget

KAMPUNI YA TBL YATOA RAI WA WADAU WA HABARI

Na MatukioDaimaAPP,Mwanza

Hayo yalizungumzwa na Meneja Mauzo wa kampuni ya bia Tanzania (TBL) Yuda Ryaga alipotembelewa na waandishi wa habari leo kiwandani hapo ikiwa ni maandalizi ya kuelekea siku ya usiku wa Waandishi na Wadau wa habari June 3 mwaka huu.


"Ningependa sana kuona siku hiyo ya waandishi wa habari kama bidhaa zote za itakuwa mezani ili wanahabari wapate nafasi ya kuonja bidhaa zetu na tunawahakikishia tu kwamba tushirikiane pamoja" alisema Ryaga


Aliongeza kuwa jamii inayoizunguka kiwanda hicho imeendelea kunufaika kwa kupata ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja kwa maana kwamba ndani ya kiwanda Kuna makapuni mengine madogo madogo ambayo yamechukua kazi ndogo ndogo ikiwemo usafi, huduma ya chakula ambao wengi waajiriwa ni wakazi wa Mwanza lakini pia wanatoa huduma ya maji ya kunywa


"Kiwanda pia kinatoa pia huduma ya maji Safi na salama ya kunywa kwa ajili ya wakazi wanaozunguka kiwanda na tunafungua tunafungua saa 12 aubuhi na kufunga saa 12 jioni ili watu waweze kupata maji Safi na salama kwa matumizu ya nyumbani," alisema Ryaga

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI