Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo Shauri Selenda ametoa nasahaa kwa jamii ili kusaidia kupambana na changamoto mbalimbali zinazowakabili watoto katika malezi.
Hayo yalisemwa na Selenda katika maashimisho ya siku ya mtoto wa Afrika katika wilaya hiyo yaliyofanyika Jana katika uwanja wa shule ya msingi Nia njema mkoani Pwani.
Moja wapo ya nasaa ni kuhakikisha uwepo wa mabalaza ya watoto ngazi ya vitongoji ,vijij hadi wilaya ili kusaidia kuwajengea uwezo watoto kujieleza pale wanapopata changamoto mbalimbali katika jamii zinazowakabili na serikali kupata Taarifa kwa urahisi na kuzifanyia kazi.
Hatuna budi kuanza kuunda mabalaza ya watoto ili wawe mabalozi wazuri katika jamii kutoa taarifa pale wanapoona Kuna viashiria vya ukatili na wanapofanyia ukatili majumbali ili kusaidia kuepuka matukio mbalimbali yanayotokea."Alisema Selenda
Watoto wengi wanafanyiwa ukatili na kuna wakati wanaona wazazi wanafanya matukio maovu lakini pale tunapohitaji taarifa zinafichwa kuanzia ngazi ya familia lakin kundi hili la watoto likipewa elimu ya utambuzi kuhusiana na haki mbalimbali za watoto na viashiria vya ukatili watasaidia kutoa taarifa mapema.
Pia ameipongeza taasisi mbalimbali zisizo za kiserikaki zinazoshughulikia masuala ya kijinsia pamoja.na watoto kwa kushirikiana na halmashauri ya wilaya Bagamoyo kuendelea kutekeleza majukumu kwa ufasaha kwa mujibu wa Sheria na utaribu na sio vinginevyo.
Tunashukuru mashirika yasiyo yakiserikaki kwa kufanya kazi nzuri katika kuelimisha jamii nakuomba kuendelea kutoa kwa jamii kupinga ukatili na kumlinda mtoto.
Naye mmoja wa wadau kutoka taasisi inayoshughilika na masuala ya ndoa, familia na malezi - TaMCare- Daktari Enock Mlyuka amesema kuwa jamii haina budi kuwajenga watoto katika malezi Bora ili kupata kizazi jwnye maadili mema na viongozi wenye uzalendo katika taifa.
'Tunatambua kwa Sasa kuna ongezeko kubwa la migogoro ya ndoa ambayo inaathiri makuzi na malezi ya watoto na familia ndio msingi wa kila kitu hivyo wakatili wanatengenezwa katika familia hivyo wakati umefika kuwekeza nguvu katika malezi bora.'"Alisema dk Mlyuka."
Akisoma Taarifa ya wilaya utekelezaji katika malezi mwalimu Sipendeki Kingwamba amesema kupitia kitengo Cha ustawi wa jamii wameendelea kutoa elimu kwa vituo mbalimbali vya kulelea watoto ili kutoa huduma Bora
Pia alitaja takwimu za mashauro mbalimbali ya ndoa kwa mwaka 2021 na namna walivyoshughuliki.
Alisema migogoro ya ndoa ilikuwa 1156, ambayo ni wanawake na watoto waliotelekezwa,migogoro ya matunzo ya watoto 288 na imesuluhishwa na kwa Sasa watoto wanapata huduma.
Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo imeazimisha siku ya mtoto wa Afrika na kuwakutanisha wadau mbalimbali wa masuala.ya jinsia na malenzi wa watoto,nakauli mbiu ya mwaka huu ni TUIMARISHE ulinzi wa mtoto,tokomeza ukatili dhidi yake,jiandae kuhesaniwa.
Mwisho
0 Comments