Header Ads Widget

HUU HAPA UFAFANUZI WA TMA KUHUSU HALI YA BARIDI NCHINI

 



Na Mwandishi wetu, Matukio Daima APP Dar es Salaam


Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania TMA inapenda kutoa ufafanuzi wa ripoti ya upotoshaji kuhusu hali ya baridi inayoendelea nchini.


Taarifa iliyotolewa na TMA kwa vyombo vya habari imeeleza kuwa, taarifa hiyo imesambaa kwenye mitandao ya kijamii ikieleza leo June 4, hadi August 22 mwaka 2022 kutakua na baridi zaidi kuliko miaka ya nyuma, taarifa hiyo imehusisha Aphelion.


Tukio la Aphelion ni hali ya kawaida katika mzunguko wa dunia kwenye mfumo wa jua (solar system), hata hivyo mchango wake katika mwenendo wa hali ya baridi kati ya msimu mmoja na mwimgine ni mdogo katika maeneo yetu kutokana na kuwa karibu na ikweta.


Kipindi cha miezi ya June Hadi August kila mwaka ni Majira ya kipupwe katika maeneo mengi nchini Tanzania ambapo mifumo ya hali ya hewa hutawaliwa na hali ya baridi na upepo mkali .


Utabiri wa msimu wa kipupwe uliotolewa na TMA tarehe 1mwezi June, mwaka 2022 unaonesha kuwa hali ya baridi ya wastani Hadi joto kiasi inatarajiwa katika maeneo mengi ya nchi ya Tanzania.


Viwango vya joto nchini vinatarajiwa kuwa kati ya nyuzi joto 14°C hadi 26°C kwa maeneo ya ukanda wa pwani kati ya nyuzi 4°C hadi 14°C kwa maeneo ya nyanda za juu kusini -magharibi na kati ya nyuzi joto 10°C hadi 20°C kwa maeneo mengine ya nchi.


Aidha, TMA imetoa tahadhari ya uwepo wa vipindi vya upepo mkali na mawimbi makubwa, tahadhari hiyo ni kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani ya bahari ya Hindi kuanzia Alhamis ya tarehe 2 na inatarajiwa kudumu Hadi tarehe 6 mwezi huu mwaka 2022 na ambayo itakua ikihisishwa kila inapobidi.


Hata hivyo, TMA inapenda kuwakumbusha kuwa kwa mujibu wa sheria ya mamlaka ya hali ya hewa Tanzania, Na. 2 ya mwaka 2019, TMA ndio Taasisi pekee yenye jukumu la kutoa taarifa za utabiri na tahadhari za hali ya hewa kwa umma, hivyo ni kosa kisheria kusambaza taarifa taarifa kutoka katika vyanzo visivyo rasmi kwa mujibu wa kifungu cha 27 na 31(5) Cha sheria hiyo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI