Header Ads Widget

HATMA YA WAKILI YABAKIA KATIKA MIKONO YA MAJAJI

 

Majaji wanaoamua kesi ya wakili wa Kenya paul Gicheru
Image caption: Majaji wanaoamua kesi ya wakili wa Kenya paul Gicheru

Mahakama ya ICC mjini the Hague Uholanzi hapo jana ilifunga kesi ya wakili Paul Gicheru kuhusu madai ya kuwahonga mashahidi ambao walitarajiwa kutoa ushahidi wao dhidi ya naibu rais wa Kenya William Ruto kuhusiana na ghasia za uchaguzi za 2007ambazo zilisababisha mauaji ya watu 1200.

Wakili wake na waendesha mashtaka wa ICC walilumbana mwisho wa kesi hiyo ambayo ilichukua takriban miezi 19, ambapo Ruto alitajwa mara kadhaa. Jaji Miatta Maria Samba alisema mahakama hiyo itajadiliana kuhusu kesi hiyo na katika wakati ufaao itatoa uamuzi wake kuhusu iwapo atakuwa hatiani au atawachiliwa huru.

Kulingana na gazeti la Nation, ofisi ya mwendesha mashtaka ikiongozwa na wakili Anton Steyberg ilisisitiza mshukiwa huyo kuwekwa hatiani lakini mawakili waliokuwa wakimtetea bwana Gicheru walikosoa kiwango cha uchunguzi na kuiomba mahakama kumuondolea kesi mteja wake.

Wakili wa Gicheru Michael Karnavas alisema kwamba ofisi ya mwendesha mashtaka haikufanya uchunguzi katika eneo la bonde la ufa , eneo ambao uhalifu ulitekelezwa , licha ya kwamba hawakuzuiliwa na serikali ya kenya.

Ikilinganishwa na kesi ya awali , ambapo eneo linalokaliwa na watu wanaofuatilia kesi hiyo halikuwa na mtu , kulikuwa na idadi kubwa ya watu waliohudhuria katika kikao cha jana ambacho kilikuwa cha mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI