Na Matukio Daima APP Dar es Salaam
Wakala wa Usajili na Wasimamizi wa Biashara Nchini BRELA wametangaza wiki ya kusuluhisha migogoro ya makampuni kuanzia leo tarehe 13 hadi 19 mwezi wa sita mwaka huu.
Akizungumza na Kaimu Mkurugenzi wa Migogoro na Majina ya Biashara Mainrad Rweymamu amesema kuwa katika zoezi hilo watakuwepo katika ukumbi wa makumbusho ya Taifa ili kusikiliza mashauri.
Amesema kuwa, kuna migogoro inatokea kwenye makampuni kwa kuwaondoa wamiliki bila taarifa na kutaifishwa kwa hisa.
"Waje kwa pamoja tuzungumze kwa pamoja tusuluhishe migogoro,wanahisa wanakufa na ndugu hawapati taarifa sahihi kuhusu hisa za marehemu"amesema Rweymamu.
Pamoja na hayo, ameyataka makampuni yatumie fursa hiyo kusuluhisha migogoro iliyopo wanafanya kazi kuanzia saa tatu hadi saa kimi na moja.
"Kampuni nyingi zipo mikoni lakini tumeanza kuzunguka mikoani kusaidia upatikanaji wa huduma tumefikia mikoa ya Tanga, Mbeya na Mwanza na huu utakuwa muendelezo "amesema Rweymamu.
Hata hivyo, amesema BRELA ndio lango la biashara nchini na migogoro ipo makampuni yajitokeze tuweze kutatua changamoto.






0 Comments