Na Gabriel Kilamlya MatukioDaimaAPP NJOMBE
Mradi Mpya wa Maji Unaofadhiliwa na Benki ya Dunia Kwa ajili ya Kupeleka Maji Katika Kata za Matola,Luponde na Uwemba Halmashauri ya Mji wa Njombe Umesababisha Upungufu mkubwa wa Maji Kwa Wakazi wa Kijiji cha Ruvuyo Kilichopo kata ya Madope Wilayani Ludewa Mkoani Njombe Kutokana na Kutega Maji Hayo Kwenye Chanzo Kimoja.
Mradi Huo Unatajwa Kusababisha Vituo 13 Vya Maji Katika Kijiji Cha Ruvuyo Ludewa Kukosa Maji Wakati wa Kiangazi Kutokana na Mgawanyo Huo Kati ya Vituo 23 Vilivyopo.
Lawama Kubwa za Wakazi wa Kijiji cha Ruvuyo Zinaelekezwa Kwa Serikali Kupitia Diwani wa Kata ya Madope Patrick Mgaya ambaye Anaeleza Chanzo cha Mgogoro Huu ambao Umekuwa Mwiba Hasa Katika Kipindi Cha Kiangazi.
Wabunge wa Ludewa Joseph Kamonga wa Kwanza Kushoto na Deo Mwanyika Jimbo la Njombe Mjini wametembelea Kijiji Cha Ruvuyo Ludewa kusikiliza kero ya Maji
Wabunge wa Majimbo Yote Mawili ya Njombe Mjini Deo Mwanyika na Joseph Kamonga Jimbo la Ludewa Kwa Pamoja Wamezulu Katika Kijiji Cha Ruvuyo na Kusikiliza Kilio Cha Wakazi Hawa.
Meneja wa Maji Kutoka Ruwasa Wilaya ya Ludewa Nasibu Mlenge amesema kuwa tayari Wataalamu wa Maji kutoka Pande Zote mbili Wameshapata Chanzo Kipya ambacho Kitaondoa Kero Hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Andrea Tsere akizungumza na Wananchi wa kijiji cha Ruvuyo amesema kuwa Maji ni Uhai hivyo Kila Mwananchi anahaki ya kuyapata kwa Usawa.
Hapana Shaka Maji ni Uhai na Pasina Maji Hakuna Uhai.
...........







0 Comments