NA HADIJA OMARY , MATUKIODAIMAAPP LINDI
Diwani wa kata ya Navanga halmashauri ya Mtama Mkoan Lindi Rashid Mkuya amejeruiwa kwa kupigwa na kipande cha Nondo sehemu mbali mbali za mwiliwake na kusababisha majeraha kichwani na kifuani na watu wasio julikana
Kwa mujibu wa Taarifa ya kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Lindi , Mtatiro Kitinkwi inasema tukio hilo lilitokea jana tarehe 12.06.2022 majira ya saa tisa usiku huko kijiji cha Mkung'uni kata ya Navanga iliyopo Halmashauri ya Mtama Mkoani Lindi
Tukio hilo limetokea wakati diwani huyo akijaribu kuokoa mali za mwananchi wake aitwaye AHMAD ALLY aliyevunjiwa duka lake na kuibiwa pesa taslimu kiasi cha Tsh. 960,000/= ,TV moja FLAT aina ya EVOLLI nyeusi yenye thamani ya TSHS. 350,000/=
Hata hivyo taarifa hiyo inasema TV hiyo alifanikiwa kuiokoa na majerhi amelazwa katika Hospitali ya MISSION NDANDA -Mkoani MTWARA
Aidha jeshi la Polisi Mkoani Lindi likishirikiana na wananchi wa vijiji jirani linaendelea kuwatafuta watuhumiwa hao.






0 Comments