Mahakama ya wilaya ya Iringa imemuhukumu Ezel Kasenegala Kifungo cha Miaka 25 au Faini ya shilingi Million 163,67000 baada ya kumtia hatiani kwa kukutwa na ngozi mbili za chui zilizokuwa na thamani ya shilingi M16,367000.Na MatukioDaimaAPP
Kasenegala ambaye ni mkulima na mkazi wa Lulanzi wilaya ya Kilolo mwenye umri wa miaka 35 alikamatwa akiwa anauza ngozi hizo kwa shilingi laki 5 kwa kila moja.
Mapema hii leo hakim mkazi mkuu Said Ally Mkasiwa amesema mtuhumiwa alikamatwa tarehe 12/05/2020 eneo la ipogolo na amekutwa na hatia ya kukutwa na ngozi mbili za chui.
Ambapo taarifa kutoka kwa wasamaria wema walilitaarifu jeshi la polisi ndipo wakaweka mtego wa kumkamata wakijifanya ni wanunuzi wa ngozi hizo za chui.
Mwendesha mashtaka wa serikali Alex Mwita ameiomba mahakama kutoa adhabu kali ili iwe fundisho kwake na jamii yenye matendo kama hayo.
Aidha mtuhumiwa ameiomba mahakama kumpunguzia adhabu kwa sababu ni kosa lake la kwanza na amefanyiwa opresheni hivyo hawezi kufanya kazi ngumu na anafamilia kubwa yenye watoto 6 na wote wanamtegemea.
Hata hivyo mahakama imemuhukumu kifungo cha miaka 25 au faini ya shilingi Million 163,laki6 77000
0 Comments