Na Fatma Ally MDTV Dar es Salaam
Watanzania wametakiwa kujenga utaratibu wa kutenga siku maalum kukaa na kuzungumza na familia zao Ili kuleta malezi bora katika familia ikiwemo kujua mienendo ya watoto wao.
Wito huo umetolewa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Maendeleo ya jamiii jinsia wanawake na wenye makundi maalum Dorothy Gwajima wakati alipotembelea katika Soko la mbezi Louis lililopo jijini humo kuelekea siku ya kimataifa ya familia duniani.
Amesema kuwa, kumekuwa na changamoto nyingi katika malezi ya watoto hali inayochangia kuongezeka kwa watoto wa mtaani na kuibuka kwa makundi ya kihalifu yasiofaa kutokana na wazazi kutokaa na familia zao kujadili mambo mbalimbali ya kifamilia.
Hata hivyo, amesema kuwa, maadhimisho hayo kitaifa yatafanyika Mkoani Dodoma, ambapo Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi, huku kila Mkoa ukitakiwa kuwa na namna yake ya kuadhimisha kwa kufanya mambo mbalimbali ikiwemo kufanya mikutano, makongamano, maandamano pamoja na kufanya michezo.
"Wazazi na walezi wanatakiwa kutenga siku maalum ya kukutana na familia zao Ili kuzungumza mambo mbalimbali ya kifamilia, kitaifa yatafanyika Mei 15 mkoani Dodoma ambapo siku hii itaangukia jumapili, siku hii sio ya kazi naomba tuitumie vizuri, leo hapa watu wamefunguka sana changamoto wanazozipitia katika familia"amesema Waziri Gwajima.
Aidha, amesema kuwa, maadhimisho hayo yamelenga kutambua umuhimu wa familia kama chanzo cha jamii katika katika kukuza familia bora zenye malezi mazuri ya kifamilia .
Ameongeza kuwa, kumekua na changamoto mbalimbali za familia ikiwemo kipato duni jambo ambalo linalisababisha kuwepo kwa migogoro na kukosa msingi wa malezi bora na kupelekea ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto.
Amesema kuwa kauli mbiu ya mwaka huu ni "Dumisha amani na upendo kwa familia imara tujitokeze kuhesabiwa"ambayo ina endana na
Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 ambayo huanzia kwenye familia.
Akizungumza na kwa niaba ya wafanyabiashara wenzake, walippo katika Soko la mbezi Mwajuma Zahoro amesema kuwa ubize katika familia unachangia kwa kiwango kikubwa kutokea kwa mmong'onyoko wa maadili kwa wototo hali inayopelekea kuongezeka kwa watoto wa mtaani.
0 Comments