Header Ads Widget

TANZANAFRICA TOURISM GROWTH WAIOMBA SERIKALI KUWASHIKA MKONO


Na Fatma Ally MDTV Dar es Salaam

Taasisi ya Tanzanafrica Toursm Growth inayojishughulisha na maswala ya usafi nchini Tanzania imeiomba Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuwaunga mkono katika juhudi wanazozifanya.


Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo, Jackline Leornad wakati alipokua katika zoezi la ufanyaji wa usafi katika fukwe za habari maeneo ya Hospital ya Aghakan iliyopo Kata ya Kivukoni Halamairi ya  Jiji la Dar es Salaam.



Amesema kuwa, kwa sasa Taasisi yao ndio inaanza kazi ya kufanya usafi katika Jiji la Dar es Salaam lakini lengo lao ni kufika katika maeneo mbalimbali ya nchi ya Tanzania lengo ni kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali katika kuhakikisha nchi hiyo inakua kinara katika masuala ya usafi.


Aidha, ameziomba Taasisi za serikali na binafsi zinazojihusisha na masuala ya mazingira kuweka ushirikiano katika zoezi la kuweka safi maeneo mbalimbali yanayosahaulika ikiwemo fukwe za bahari.


"Tunaziomba taasisi zote za Serikali na Binafsi  kuunga mkono juhudi zetu kwa kushirikiana katika shughuli hizi, ambapo amesema  kuwa zoezi hili litakuwa ni endelevu kufanya usafi maeneo mbalimbali ili kuweza kuweka mazingira safi salama ili kuvutia watu kutalii maeneo ya vivutio"amesema Jackline.


Kwa upande wake Mtendaji wa Mtaa See view Kata ya Kivukoni, Ashura Bwatamo ameiomba serikali kwa kushirikiana na wadau muhimu kujitokeza kuwasaidia kupata vifaa kwani wanakabiliwa na changamoto ya uhaba wa vifaa vya kufanyia usafi.


Aidha, mempongeza Mkurugenzi wa Taasisi ya Tanzanafrica Toursm Growth kwa kujitolea kufanya usafi katika maeneo ya Mtaa huo kwani itachangia kuweka mazingira safi na salama, huku akiwataka wadau wengine kufika katika daraja la Tanzanite kufanya usafi kutokana na uchafu mwingi wa Chupa nyeusi uliopo chini ya daraja Hilo.

"Tunashukuru sana kwa wadau kujitokeza kama hivi katika maeneo yetu kufanya usafi, lakini naomba wadau wengine wajitokeze pale chini ya daraja kuna Chupa nyingi nyeusi wanaokota makopo wanasema zile hazina faida kwani haziwezi kurejelesheka tena kiwandani, tunaomba wadau waje wazitoe "amesema Ashura.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI