MKUU wa mkoa wa Iringa Queen Sendiga ametangaza kuwasaka wale wote wanaojihusisha na vitendo vya ukatili ndani ya mkoa huo.Mwandishi Francis Godwin Matukio DaimaAPP
Akizungumza na wanahabari ofisini kuhusiana na siku ya familia Duniani inayofanyika kila mwaka Mei 15 ,alisema mkoa wa Iringa umejiwekea mikatika kabambe ya kukomesha Matukio ya ukatili yanayojitokeza kwenye jamii na kutaka wananchi wasikubali kufumbia macho vitendo vyovyote vya ukatili kwenye maeneo yao .
Sendiga alisema kutokana na elimu inayoendelea kutolewa dhidi ya ukatili ndani ya mkoa wa Iringa idadi ya wanaume wanaofika dawati la jinsia kulalamika kufanyiwa ukatili na wake zao imeongezeka tofauti na mwanzo ambapo wanaume walikuwa wakiona aibu kwenda Polisi kutoa taarifa za wao kufanyiwa ukatili na wanawake.
"Tunapoona wanaume wanajitokeza kwenda dawati kulalamika kufanyiwa vitendo vya ukatili tunaamini elimu imefika na ni mwanzo mzuri wa Matukio ya ukatili kuendelea kupungua mkoani kwetu"
Hata hivyo alisema bado ukatili Kwa wanawake na watoto umeendelea kuwepo japo si Kwa kasi kubwa kama zamani na kutaka jamii kuendelea kuwaibua wanaofanya ukatili .
Mkuu wa mkoa alisema iwapo wazazi watazingatia ushauri mbali mbali unaotolewa na Viongozi wa Serikali na vyombo vya usalama Kuhusu uangalizi wa watoto wao itasaidia kupunguza kabisa Matukio ya ubakaji,ulawiti na mengine Kwa watoto nyakati za usiku .
Kwani alisema vitendo vya baadhi ya wazazi ama walezi kuwatuma watoto usiku kwenye madukani ni moja ya sababu inayochochea ubakaji na ulawiti Kwa watoto nyakati za usiku .
Katika hatua nyingine mkuu huyo wa mkoa alisema ukatili wa baadhi ya wanaume hasa wanaolewa kupindukia kunyonya Maziwa ya wake zao wanaonyonyesha Kwa Imani ya kukata pombe unaendelea kupungua na kuwashauri wanaume hao kuacha tabia hizo.
0 Comments