Header Ads Widget

ASEMAVYO RC SENDIGA BAADA YA KUTIMIZA MWAKA MMOJA IRINGA



SIKU 365 : 

Asante Mungu Baba wa Mbinguni kwa neema,baraka na ulinzi wako,Sifa na Utukufu zinarudi kwako.

Kwa unyenyekevu mkubwa napenda kurudisha shukrani za dhati kwa Mh. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kua na imani kubwa ya utumishi wangu kwa wananchi.


Nawashukuru watumishi wenzangu wote kuanzia ngazi za juu mpaka  Mkoa wa Iringa,kwa pamoja mmekua wema sana kwangu kuanzia siku niliyokanyaga ardhi ya Iringa hadi sasa,mafanikio tunayoyapata si kwa sababu yangu pekee bali ni yetu wote kwa kupambana usiku na mchana kuwatumikia wananchi wa Iringa,nasema asante sana.


Mwisho niwashukuru wananchi wa Mkoa wa Iringa walio ndani ya Iringa na walio nje ya Iringa kwa umoja wao na kuzidi kunipa moyo kila kukicha hivyo kunifanya kuamka na nguvu ya kuendelea kuwatumikia zaidi kunionyesha Upendo.


Asante sana Serikali Awamu ya Sita. Asante sana Mwenyezi Mungu na hivyo basi kazi iendelee


Uwajibikaji rafiki wa maendeleo 

#Siku365zaQueenSendiga

#Utumishi

#Iringa woodland 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI