Header Ads Widget

SHEIKH MKUU WA MKOA WA MWANZA AMEWATAKA WAISLAMU WOTE KUYAENZI YALE YOTE WALIOJIFUNZA NDANI YA RAMADHANI.

 


NA CHAUSIKU SAID , MATUKIODAIMAAPP MWANZA 

Waumini wote wa dini ya kiislamu wametakiwa kuyaenzi matendo yote mema waliyokuwa wakijifunza katika mfungu wa mwenzi mtukufu wa Ramadhani.

Hayo yamebainishwa hivi leo na sheikh Mkuu wa Mwanza Hassan Kabeke wakati akizungumza na waandishi wa habari na kuwataka waislamu wote kuyaendeleza matendo mema baada ya mfungo kuisha.

Kabake ameeleza kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kuendelea kuyaishi yale yote waliyokuwa wakiyaishi katika kipindi cha Ramadhani na hata katika kipindi hichi ambacho mwezi mtukufu unaisha.

"Kwa kawaida ndani ya Ramadhani tumeswali swala tano bila kukata,  tumetoa sadaka pamoja na kuwahurumia watu hivyo tunapsawa kuendelea hivyo" Alisema Kabeke.

Amefafanua kuwa ni aibu kwa muumini wa kiislamu baada ya siku mbili mfungo kuisha anakutwa mtaani amelewa, na kuwa na wanawake ambao si halali katika dini badala ya kuendelea kuenzi yale mambo aliyojifynza katika mwezi mtukufu.

Kabeke ameeleza kuwa kutokana na Baraza la Idd kufanyika kitaifa ambapo mgeni rasmi atakuwa Rais wa jamhuri wa Muungano wa Tanzania Samia Suluhu hivyo baraza hilo halitafanyika kimkoa,  hivyo waumini wote watafatilia katika runinga.

Aidha amewataka wamiliki wa mashule na vyuo kuwaruhusu vijana wa kiislamu kwenda kuswali swala ya idd pamoja na masheikh watakaoswalisha siku ya idd waweze kuimiza ujenzi wa vituo vya afya ambapo kila wilaya kitajengwa kituo cha afya kimoja.

"Tayari tumeanza ujenzi huo na unaendelea na tumejipanga kufanya harambee tarehe 30 julai" Alisema Kabeke.

Ametoa wito kwa wazazi kuhakikisha wanasherekea sikukuu pamoja na watoto wao na sio kuwaacha peke yao na kwenda katika kumbi za starehe.

Hata hivyo sheikh kabeke amewakumbusha waumini wote wa kiislamu kuwa swala itafanyika katika viwanja vya nyamagana wilaya ya Nyamagana

Kwa upande wake Hamad Nchola ambae pia ni muumini wa dini ya kiislamu amewataka waumini wenzake kisherekea kwa amani bila kufanya fujo za aina yeyote ile ili kuendeleza amani ya nchi .

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI