Header Ads Widget

NIKONEKT APP KUTATUA KERO KWA WATEJA

 


Na Pamela Mollel,Arusha 


Shirika la umeme Tanzania limezindua mfumo mpya wa NIKONEKT APP kwaajili ya kutoa huduma kwa wateja kwa njia ya kidijitali


Akizungumza hivi karibuni Meneja  wa Tanesco Mkoa wa Arusha Mhandisi Herini Mhina katika semina ya siku moja ya kuwapa uelewa wakandarasi juu ya  mfumo huo 



Alisema kuwa kupitia mfumo huo wa kidijitali utakwenda kuondoa changamoto mbalimbali na za mda mrefu ambazo zilikuwa zikiwakabili wateja


"Kwa mfumo ulivyo utaongeza uwazi zaidi na kutatua kero za vishoka ambao walikuwa wakisumbua wateja na kusababisha hasara kubwa "Alisema Mhandisi Mhina


Aliongeza kuwa kwa namna mfumo unafanya kazi utakwenda kumrahisishia mteja kufanya huduma akiwa nyumban kwa tumia simu ya mkononi 


Kwa upande wake meneja wa EWURA Lorivil Longidu alipongeza shirika hilo kwa kuja na ubunifu mkubwa wa kuanzisha mfumo huo ambao utakaokwenda kutatua changamoto za wateja


Alisema kuwa kazi zote za ufundi wa umeme zitafanywa na wakandarasi au watu wenye leseni za EWURA 


Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI