Mkurugenzi Mkuu wa Taasis ya Utafiti wa Kilimo TARI Dkt. Geoffrey Mkamilo akiongoza wakurugenzi wengine wa TARI Zephania Mshanga, Dkt. Joel Meliyo na Dkt Juliana Mwakasendo walipotembelea ofisi ya Makao Makuu ya Jeshi la Magereza Tanzania lililopo Msalato Dodoma ili kujifunza na kuona shughuli zinazofanywa na Jeshi hilo kama hatua za kuelekea kusaini mkataba wa mashirikiano kati ya taasisi hizi mbili.
Dkt Mkamilo amemhakikishia "Commissioner General of Prisons" CGP M Mzee kuwa TARI ipo tayari kufanya kazi kwa ukaribu na Jeshi la Mageraza kwenye masuala mbalimbali kama uzalishaji wa mbegu, utafiti, usambazaji wa teknolojia za kilimo.
Aidha Dkt Mkamilo amewapongeza Jeshi la Magereza kwa kazi nzuri wanazofanya hasa upande wa kilimo mfano uzalishaji wa miche ya michikichi Kigoma kupitia Gereza Lakwitanga.
Naye Kamishina general wa Jeshi la magereza nchini Meja general " CGP Mzee (ndc) amesema amefurahi kutembelewa na TARI amepata nafasi ya kujifunza shughuli zinazofanywa na TARI na ameahidi kuendelea kushirikiana ili kulima kwa kufuata ushauri wa kitaalam ili kilimo kiwe na tija na hivyo kuongeza uzalishaji na hivyo Jeshi linaweza kujitegemea
0 Comments