Header Ads Widget

MFANYAKAZI WA NDANI ATIWA MBARONI KWA TUHUMA ZA KUMUUA MWANAE BAADA YAKUJIFUNGUA

Na Frederick Siwale - Matukio daima tv Makambako Njombe.      

Msichana mmoja mfanyakazi wa kazi za ndani aitwaye Tumsifu Kihombo (16) mkazi wa mtaa wa Kahawa kata ya Kitisi Halmashauri ya Mji Makambako Mkoani Njombe ,amekamatwa kwa tuhuma za kujifungua mtoto na kumuua kwa kumnyonga shingo kwa kutumia kipande cha kanga na kuuficha uvunguni mwili wa kichanga hicho.                


Akizungumza na Matukio daima tv Mama mwenye nyumba ambaye ndiye boss wa mtuhumiwa aitwa Anna Mdindile (45) alimtaja mtuhumiwa kuwa ni Tumsifu Kihombo (16)  mfanyakazi wa ndani .                                 


Bi. Mdindile alisema mtuhumiwa alifika katika mtaa huo kama mfanyakazi wa ndani nalitafutiwa kazi na Shangazi yake mkazi aitwaye Samwenudzi Kihombo (75) kwa madai ya kuwa mtuhumiwa ni yatima ambaye hana baba wala mama na amelelewa na yeye Shangazi yake hadi aliposhindwa kuendelea na masomo akiwa kidato cha pili katika shule ya Sekondari Ibumila iliyopo katika Halmashauri ya mji wa Makambako.               


"Huyo mtoto nilipokea na nimeishi naye kwa kipindi cha mwaka mmoja tu na sikuwahi kuona kama alikuwa mjamzito hadi Jumapili mei 08 /2022 lilipotokea tukio hili la kusikitisha" Alisema Bi.Mdindile.


Siku ya tukio alisema alishituka kuona hadi saa 4 :15 asubuhi dada wa kazi hajatoka chumbani kwake ili hali haikuwa kawaida yake kulala hadi muda huo na mara nyingi siku za Jumapili hutangulia Kanisani na Watoto wa Mama mwenye nyumba lakini siku hiyo Watoto hao mmoja mwenye umri wa miaka 6 na mwingine miaka  9 walikwenda peke yao.    


" Haikuwa ajabu sana watoto kwenda peke yao Kanisani KKKT Usharika wa Mjimwema kwa kuwa ni jirani na nyumbani ni mita 300 tu, lakini nilipatwa na hofu kusikia sauti ya mtoto mchanga akilia kutoka katika chumba hicho na nilipomuita Tumusifu aliitika na kusema kichwa kinaniuma na nilipomuuliza sauti ninayoisikia ni ya mtoto wa wani alinijibu kwa kukataa kuwa mbona yeye yuko peke yake na nilipomtaka afungue mlango alikataa na kusimama nyuma ya mlango kuziba nisione  ndani.Alisema Bi.Mdindile.                     


Baada ya kuona hali hiyo alisema aliamua kwenda kutoa taarifa kwenye Uongozi nyumbani kwa balozi ambapo balozi Bw.Joseph Kifikilo (67) alifika kwa kushirikiana na majirani walimlazimisha mtuhumiwa kufungua mlango na alipofungua walikuta damu nyingi ikiwa imetapakaa sakafuni .           

Alipoulizwa kuhusu damu hiyo mtuhumiwa alidai kuwa yupo hedhi na ndipo walipo pata mashaka zaidi wakaamua kufunua godoro na chaga za kitanda na kugundua mwili wa mtoto mchanga ukiwa nje ya nyumba ya uzazi ukiwa umefungwa na kipande cha kanga shingoni.                           


Balozi Bw.Joseph Mfikilo alisema ilimlazimu kujulisha Uongozi wa Serikali ya mtaa kwa afisa mtendaji wa Kahawa Bi.Devota Nestory ambaye alifika na kutoa taarifa kituo cha Polisi Makambako kwa hatua zaidi.                 


Afisa Mtendaji ambaye hakutaka kupigwa picha alisema tukio hilo ni la kweli na inaonekana mtoto huyo ameuawa kwa kunyongwa kwa kutumia kipande cha nguo .                                 


" Mwandishi wa habari mtuhumiwa mwenyewe anakili kuwa alijifungua salama na aliamua kumnyonga kwa kutumia kanga baada ya kubaini kuwa boss wake ameshitukia tukio zima na hivyo kuamua kupoteza ushahidi" Alisema afisa mtendaji huyo.         

Aidha alisema yeye Mtendaji kama mlinzi wa amani katika eneo hilo alipomhoji mtuhumiwa alijibiwa kiwa alifanya hivyo ili usiku ungefika angeuweka mwili wa kichanga huyo ndani ya boksi na kwenda kuutupa jalalani.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI