Na, Mwandishi Wetu, Kagera.
Viongozi pamoja na wadau wa taasisi Tanzania Peace Foundation TPF mkoani kagera wamefanya matembezi maalumu ya kutembelea jumba la makumbusho Mushonge iliyopo kata ya kamachumu tarafa kamachumu mkoani Kagera.
Akizungumza na waandishi wa habari katibu mkuu vijana Taifa Charles Sabiniani maarufu kama Lowasa amesema kuwa, wamefanya matembezi hayo kama sehemu mojawapo ya kumuunga mkono rais Samia Suruhu Hasan ya kuimiza utalii nchini.
"kwelikweli kama kiongozi wa kitaifa kutoka tpf ninaekutana na vijana mikoa mbalimbali vijana wanajivunia na uongozi wa Rais mimi charles sabiniani ni mjasiriamali niliewai kufanya kazi na makampuni mbalimbali ya nje naona kabisa marafi wa nje kupitia tanzania royal tour wanaulizia tanzania na kuvutiwa kuja tanzania ivyo naona kabisa juhudi za Rais wetu Mpendwa kazi hii aliyo ifanya Samia Suluhu Hassan ni kazi ya kizalendo iliyo tukuka kabisa"
Aidha, amesema kuwa vijana wa TPF nchini wanaimani na viongozi wa serikali ya sita kwa uchapakazi uliotukuka hasa katika kuimiza uchapakazi na uzalendo ili kudumisha amani katika nchi, na kusema kuwa matembezi waliyoyafanya yamewasaidia sana kuijua historia ya mkoa wa Kagera.
"Niliwaalika viongozi wa tanzania peace Foundation mkoa Kagera na wenyeji wao wilaya Muleba tulitembelea nyumba hii ya makumbusho mushonge iliyo ifadhi zana mbalimbali za jadi zilizotumiwa hapo zamani nyumba hii iko mkoani Kagera wilaya muleba kata kamachumu tulipo fika tumepata historia ya kabira la wahaya na dhana walizo tumia enzi hizo ivyo wageni waalikwa wamejifunza mengi tumefanya ivi kama sehemu ya ya kumuunga mkono Rais wetu Samia Suluhu Hassan mwanamke anaechapa kazi kwa kasi " Alisema Sabinian.
Sambamba na hilo, amewaomba watanzania wote tuendelee kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na viongozi wake waandamizi na kuepuka kujiingiza kwenye mambo yasio mpendeza Mungu ili baraka ziendelee kushuka nchini Tanzania.
0 Comments