Header Ads Widget

JUKWAA LA WALIMU WAZALENDO LAMPA TANO RAIS SAMIA

 




Na Fatma Ally MDTV Dar es Salaam


Jukwaa la Walimu Wazalendo Tanzania limempongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwakuongeza mshahara wa watumishi wa Umma kwa asilimia 23.3, kukuza Utalii pamoja kupandisha madaraja kwa walimu.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Katibu  Mkuu wa Jukwaa hilo, Anuwary Ally amesema kuwa Rais Samia amefanya mambo makubwa katika Taifa lake licha ya kuingia madarakani katika kipindi ambacho nchi inapitia athari za ugonjwa wa corona.


Amesema kuwa, ongezeko la asilimia 23.3 linakwenda kuchochea ukuaji wa uchumi wa Taifa na mtu mmoja kwa kuongeza mzunguko wa fedha  kwa wananchi.


"Licha ya changamoto zote hizo za kuathirika kwa uchumi wetu,lakini Rais Samia ameuhami uchumi wetu na ameweza kuongeza mshahara kwa kiwango kikubwa, hakika anastahili pongezi na kutiwa moyo"amesema Anuary.



Sambamba na hayo, amesema kuwa, licha ya kupandishwa mishahara ameweza kupandishwa vyeo/madaraja zaidi ya watumishi 190,781 ambapo ametumia zaidi  ya shill bill 39 sambamba kulipa madeni ya mishahara wa Umma 65,394.


Ameongeza kuwa, pia katika Sekta ya Elimu amejenga madarasa 15 hali ambayo imechangia wanafunzi wote kuingia shule kwa wakati mmoja.


Amesema kuwa, Rais Samia amefanya uzalendo kwa kufanya filam ya Royal Tuor ambayo inakwenda kutangaza fursa za Utalii, itavutia watalii wengi zaidi kutembelea Tanzania, na wawekezaji na itakua uchumi wa Nchi ya Tanzania.


Hata hivyo, amesema kupitia klabu za uzalendo tutawaandaa wanafunzi kuwa mabalozi wazuri wa filamu ya Royal Tuor kwa kuwaelezea maana yake, umuhimu wake, faida zake kwa mtu mmoja mmoja.



Amesema pia wataendelea makongamano ya Royal Tuor, kuanzia ngazi ya chini kabisa kwenye Kata ambapo zoezi hilo litafanywa na wanajukwaa wote kutoka mikoa, lengo ni kuendelea kuisemea, kuitangaza na kutoa elimu kwa jamii ya chini ambayo inapaswa kujua ya Royal Tuor na umuhimu wake.


Aidha, ametoa wito kwa watanzania kujitokeza kwa wingi kuhesabiwa kwa wakati sensa itakapoanza, ambapo itasaidia Serikali kurahisisha shughuli za maendeleo.


Hata hivyo, pia wamezindua kauli mbiu yao itakayoonesha ni kwa namna gani wanamuunga mkono Rais Samia ambayo ni "NASIMAMA NA MAMA".


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI