Mkuu wa Chuo Cha Kilimo Cha Kilimanjaro (KATC) Nikodemas Shauri Tanga ameelezwa majukumu ya chuo hicho Cha Kilimo kuwa ni kuendeleza wakulima wa skimu wa lower Moshi ili waweze kuzalisha mazao mbalimbali kwa ustadi.
Amesema kuwa pamoja na kifundisha wakulima pia wanawaandaa vijana watakaoenda kuwa mabwana shamba katika tasisi za Serikali na tasisi binafsi pamoja na makampuni ya watu binafsi au kujiajiri wenyewe.
Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Kilimanjaro Mkuu huyo amesema kuwa tangu mwaka 2007 Serikali imekuja na azimio la kuwa na bwana shamba mmoja katika Kila Kijiji na kusema Kila kituo Cha Serikali Cha Wizara ya kilimo ikapewa jukumu la kifundisha mabwana shamba.
"Ndipo na sisi tulipopewa jukumu la nyongeza la kifundisha mabwana shamba katika ngazi mbalimbali na kwa hiyo toka wakati huo tumekuwa tukifundisha mabwana shamba na mpaka Sasa tuna wanafunzi wa ngazi tofauti wanaoendelea kusoma hapa"Alisema.
ameendelea kusema kuwa uwezo wa chuo hicho kuchukua idadi ya kubwa ya wanafunzi ni ndogo ukilinganisha na vyuo vyingine ambapo amesema kuwa wapo katika harakati za kuongeza miundombinu ambayo itawawezesha kuongeza idadi ya wanafunzi .
Hata amesema kuwa lengo la chuo hicho ni kufikia malengo kwa ndani ya miaka miwili au mitatu wawe wameweza kufikia uwezo wa kudahili wanafunzi miambili.
0 Comments