Na Chausiku Said Mwanza.
Taasisi ya PASS imekutana na wadau mbalimbali wakiwemo sekta ya kilimo hapa Jijini Mwanza ikiwa na lengo la kuongeza uelewa juu ya Taasisi hiyo namna inavyofanya kazi.
Akizungumza Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara Adam Kamanda ameeleza kuwa PASS imeishawanufaisha jumla ya wajasiliamali Mil1.7 ambao wamenufaika na mikopo yenye thamani ya trilion 1.219 kutoka taasisi mbalimbali za kifedha.
Kamanda ameeleza kuwa ili kuendana na mabadiliko ya teknolojia yenye lengo la kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wakulima nchini.
Amesema kuwa pamoja na kuwarahisishia huduma wanufaika huduma pia wamekuwa sehemu ya mkakati wa Taasisi katika juhudi za kihimiza ukuaji wa kijani shirikishi unaolenga kuhamasisha utunzaji wa mazingira kwa kilimo endelevu na uchumi.
"Ndio maana unaona pia tunatoa zawadi ya miche ya miti, lengo ni kuhakikisha tunaborsha huduma za kilimo huku tukienzi mazingira yetu" Alisema Kamanda.
Aidha ameeleza kuwa moja ya kanda muhimu katika sekta ya kilimo nchini kutokana na takwimu za mwaka jana 2021 pekee jumla ya wakulima na wajasliamali 37, 717 ambao kati yao 12, 277 ni wanawake na wanaume 25, 440 walinufaika wa huduma.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Robert Gabriel ambaye pia alikuwa mgeni rasmi ameeleza kuwa serikali ya mkoa huo inatambia huduma zinazotolewana na PASS ikiwemo udhamini wa mikopo kwenye taasisi za kifedha pamoja na maandiko yenye sifa zinazokubarika katika mabenki yanayowezesha wakulima, wafugaji na wavuvi kupata mikopo.
Gabriel amesema kuwa mkutano huo utasaidia kuchochea maendeleo kwa wananchi na kuchangia katika jitihada za kupunguza umaskini, kwa kuongeza uelewa, kuhamasisha wananchi kuhusu fursa zilizopo katika taasisi ya PASS.
"Hii ni nafasi kubwa ya kujadiliana na kupanga mipango na mikakati ya kutatua changamoto zinazowakabili wakulima, wafugaji, wavuvi pamoja na wasindikaji, kwa hiyo nawasaa wananchi wa Tanzania ichukulieni Taasisi ya PASS kuwa ni fursa" alisema Gabriel.
Amefafanua kuwa PASS itawezesha kitengeneza mazingira yatakayoweza kubaini changamoto na kuendelea kuweka mazingira rafiki ya kikabiliana nazo na kufikia mapinduzi ya kilomo katika Mkoa .
Hata hivyo ameeleza kuwa mbali na uzalishaji mkubwa wa mazao bado zipo changamoto zinazoikabili sekta ya kilimo ikiwemo pamoja na uzalishaji mdogo wenye tija hafifu kutokana na wakulima , , wavuvi, wafugaji, pamoja na wafanyabiashara kuwa na mitaji midogo.
Kwa upande wake Happness Kishoa ambaye ni mnufaikaji wa PASS ameeleza kuwa hakuwa na mtaji wa kutosha na hivyo Taasisi hiyo ilimsaidia pesa kiasi cha shilingi Mil15 ambazo zilimsaidia kuendeleza ufugaji ambapo awali alikuwa na mifugo michache na kwa sasa amefikisha mifugo takribani 100.
0 Comments