Header Ads Widget

MAONYESHO YA BIASHARA KWA NCHI ZINAZOZUNGUKA ZIWA TANGANYIKA KUANZA KIGOMA

 


Na Editha Karlo,Matukio Daima APP Kigoma


MAONYESHO ya biashara kwa nchi zinazozunguka ziwa Tanganyika yanatarajiwa  kuanza leo mjini Kigoma ambapo asilimia 90 ya wajasilimali kutoka katika nchi hizo wamethibitisha kushiriki.


Mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara, wenye viwanda na kilimo (TCCIA), Abdul Mwillima alitoa taarifa hiyo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya maonyesho hayo ambayo ni sehemu ya kongamano la wafanyabiashara kutoka kwenye nchi hizo.


Mwillima alisema kuwa wamefanya mawasiliano na vyama vya wafanyabiashara kwenye nchi hizo wamethibitisha kushiriki maonyesho hayo sambamba na kongamano la wafanyab iashara litakalofanyika kuanzia Mei 9 mwaka huu.


Mwenyekiti huyo alisema kuwa kufanyika kwa maonyesho hayo na kongamano la wafanyabiashara kunaenda kutengeneza uchumi mkubwa kwa mkoa Kigoma ambao utaimarisha uchumi wa mkoa na watu wake.


Akizungumza kwenye mkutano huo Afisa Biashara sekretariet ya mkoa Kigoma, Deogratius Sangu alisema kuwa wamewasiliana na Balozi za Tanzania kwenye nchi zinazoshiriki maonyesho na kongamano hilo ambao wamethibitisha kuwa na idadi ya wafanyabiashara watakaoshiriki maonyesho na kongamano la wafanyabishara.


Sangu alisema kuwa ujumbe wa kongamano hili lina ujumbe unaosema Mipaka yetu kukuza uwekezaji na biashara jumbe ambao unatoa nafasi kubwa kwa mkoa Kigoma katika utekelezaji wa mkakati wa biashara za kuvuka mpaka kwenda nchi hizo zilizo kwenye mwambao wa ziwa Tanganyika.


Afisa biashara huyo wa mkoa alisema moja ya fursa kubwa katika utekelezaji wa mpango huo ni kujiunga na nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) katika Jumuiya ya Afrika Mashariki jambo ambalo linatoa tija kubwa kwa wafanyabiashara na wajasilimali wa mkoa Kigoma.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI