Header Ads Widget

HALMASHAURI ZITENGE BAJETI ZA MBEGU ZA MUHOGO

  



Na Mwandishi, wetu


Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (Tari Naliendele) wametoa ushauri kwa Halmashauri Mkoani Ruvuma kutenga bajeti kwaajili ya kuandaa mbegu za muhogo kwa wakulima ili ziweze kuwafikia kwa urahisi zaidi. 


Akizungumza wakati wa siku ya mkulima shambani Julius Butindi kutoka idara ya  uhaulishaji wa teknolojia na mahusiano Tari Nalindele alisema kuwa wakulima wamepata elimu kutoka kwa watalaamu wa zao la muhogo ambapo Halmashauri zinawajibu sasa wa kuhakikisha kuwa mbegu zinawafikia wakulima kwa urahisi kwa kutengea bajeti. 


"Tunapotoa elimu kwa mkulima huwajibika kuanzia kulima hadi kuvuna na kisha kuzichemsha na kuwapa uhuru wa kuchagua mbegu gani bora itawafaa mbegu hizi ni mbegu zinazovumilia magonjwa na ukame pia hizi mbegu kwao ni fursa kubwa”


Kazi yetu kubwa ni kuhakikisha teknolojia zote zilizopo kwa watafiti tunazitoa kwao na kuzipeleka kwa watumiaji kwakutumia mbinu mbalimbali ikiwemo media na kuandaa siku za wakulima kama leo na kujumuika nao”


“Lengo ni kuwe na tija kubwa kwenye mazao mbalimbali ikiwemo zao hili la muhogo ndio maana tunazishirikisha ambalo ni zao muhimu kwa nchi ambalo litaongeza tija kwa wakulima na kuongeza uzalishaji na upatikanaji wa muhogo nchini” alisema Butindi 


Nae Zaituni hussein mkulima wa zao la muhogo kutoka kijiji cha Mpandangindo halmashauir ya wilaya ya Songea alisema kuwa wakulima wengi wanahitaji mbegu ili kuweza kulima zao hilo. 

Kama watakuwepo wa zalishaji wa mbegu sawa lakini kama hawapo tunaomba Tari muangalie namna ya kutusaidia ili tuwez  kupata mbegu hizo ambazo kwetu ni fursa kubwa na tunaamini kuwa itakuwa msaada kwetu baada ya mbegu ya mbolea kupanda”


Nae Ratifu Millanzi alisema kuwa mbegu hizi ni nzuri zitafaa kwa wakulima ambao ni wafanyabishara na zitafaa kwa mavuno muhimu zipatikane kwa wakati na zisogezwe kwetu. 


“Hii mihogo ni mizuri nimeijaribu nimeona inafaa kwa kilimo na kuuza ili tuweze kuinua pato letu kiuchumi ujio wa mbegu hizi utakuwa chachu kwetu utakuwa ni fursa pekee kwetu tunaimani wataaalamu wetu watatuwezesha kupata mbegu hizo”

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI