Na Andrew Chale,Matukio DaimaAPP Zanzibar.
GARI dogo aina ya Nissan Juke yenye namba za usajili Z 900 LZ iliyokuwa ikiendeshwa na mmiliki wake aliyefahamika kwa majina, Bi. Zawadi Johakim, mkazi wa Michenzani amenusurika kifo kufuatia gari hiyo kupata hitilafu na kuwaka moto.
Akielezea tukio hilo usiku huu mara baada ya kushuhudia gari lake hilo kuteketea lote kwa moto huku yeye na familia yake wakifanikiwa kutoka salama, Bi. Zawadi alisema kuwa,
Aliona moshi pembeni ya taa ndipo alipotafuta eneo la kupaki ilikuangalia tatizo lakini kabla hawajashuka moto ukaanza kuwaka pembeni mwa taa na kuanza kushika moto gari nzima na kuanza kushuka haraka.
"Baada ya kuona moshi, nilijitahidi kutafuta eneo la kuliegesha 'parking', nilikuwa kwenye foleni ndo nikatafuta parking na kuilega hapa lakini ile kitendo cha kuparking ndipo ikaendelea kushima moto.
..kabla hatujashuka gari likaanza kuwaka pale kwenye ile taa ya mbele nikamshusha mtoto wangu, kwa kuwa mvua inanyesha nikahisi bati la gari ilikuwa ime 'heat joto'. Tukaweka pembeni na kuzidi kuwaka moto ndani ya gari tulikuwa wanne watoto wangu." Alisema Bi. Zawadi.
Aidha, alisema kuwa licha ya kujaribu kuuzima na kifaa cha kuzimia ndani ya gari, lakini moto huo uliweza kushika kwa haraka na kuunguza gari lote.
"Nawashukuru watu wa Kikosi cha Zimamoto, licha ya changamoto waliweza kufika, ingawa walikutana na foleni barabarani, wameweza kuzima moto iliusiunguze majengo na maduka ya jirani.
Pia Nawashukuru wananchi kwa kutusaidia licha ya gari kuungua lote" alisema Bi. Zawadi.
Hata hivyo, Bi. Zawadi alisema kuwa anashukuru Mungu wametoka salama yeye na watoto wake na mengine anamuachia Mungu huku akiwashauri Wananchi wengine wanaomiliki magari kuwa na kifaa cha kuzimia moto 'Fire Extinguisher'.
Hata hivyo, awali mtandao huu wa Matukio Daima, umeshuhudia changamoto kwa magari ya Kikosi cha zimamoto na Uokoaji (KZU), wakishindwa kufika kwa wakati kutokana na changamoto za msongamano wa magari.
Ambapo gari hizo za Vikosi vya zimamoto zaidi ya mbili zilikutana na changamoto kufika eneo la tukio baada ya barabara kuwa na msongamano mkubwa wa magari ambapo mengi wakiwa katika sherehe za Sikukuu ya Eid.
Gari zaidi ya mbili za KZU 266 na KZU 271 ziliweza kukumbana na changamoto hiyo ya foleni huku wakipambana kusogea kwenye ajali hiyo na kupambana kuzima moto huo.
Hata hivyo, watendaji wa KZU hawakuwa tayari kuzungumzia suala hilo ambapo taarifa rasmi wanakusudia kuitoa mapema hapo baadae.
0 Comments